CCJ
Mlolongo wa Habari kuhusu Chama Cha Jamii (CCJ)

Sitta, Dk. Mwakyembe hawatoki CCJ - Ng’hily
ANAJIAMINI na anasema anaweza kusimamia kile anachokiamini.
Walioanzisha CCJ wafukuzwe uongozi
UTAWALA wa Rais Jakaya Kikwete umekumbwa na misukosuko mingi, lakini zimekuwepo fursa kadhaa ambazo kama angezitumia vema zingeleta unafuu katika utawala wake.
Wakati wa sakata la mkataba wa Richmond lililosababisha aliyekuwa waziri mkuu wake Edward Lowassa kujiuzuru na hivyo kuvunja baraza zima za mawaziri, ilikuwa ni fursa adimu kwa Kikwete kubadili sura na muundo wa baraza lake ili kujipanga upya.

Prof. Safari: Saa ya ukombozi ni sasa
UAMUZI wa mwanaharakati maarufu wa haki za waislamu, Profesa Abdallah Jumbe Safari (59) kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), umetikisa siasa za Tanzania.

Sitta kung’olewa uspika
KUNA njama za kuwatoa “kafara” wabunge 15 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kusafisha njia ya urais wa Edward Lowassa, MwanaHALISI limeelezwa.

Rostam atumbukiza CCM katika tope
- Sakata la Mpendazoe
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeingizwa kwenye tope. Gazeti la mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, Rostam Aziz limemzulia uwongo Rais Jakaya Kikwete.

CCM imelogwa na CCJ
KATIKA siku za hivi karibuni tumeshuhudia vituko na maajabu, na sitashangaa iwapo siku si nyingi zijazo tutaona miujiza.

CCJ wakana ushoga
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Jamii (CCJ), Renatus Muabhi amekana kuhusika na vitendo vya ushoga.

Kikwete atishia wenzake
- Wapanga kuhama chama
- Aliyotabiri Mkapa yaja
BAADHI ya viongozi na wanachama mashuhuri ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana mpango wa kuanzisha chama cha siasa ili kuweka upinzani mkali kwa Rais Jakaya Kikwete ifikapo 2010, MwanaHALISI limeelezwa.