Kikwete
Mlolongo wa Habari zinazomhusu Rais Kikwete

Kikwete amtosa Warioba
CCM Trust ni moja ya makampuni manne yanayounda kampuni ya Mwananchi Trust Limited yenye hisa katika kampuni ya Mwananchi Gold Limited (MGL) ya Dar es Salaam.

‘JK anavunja Katiba’
DK. Willibrod Slaa amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda.

Kikwete aingia tope jipya
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete yaweza kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine. Mara hii kwa kushindwa kutoa malipo yanayohusiana na uzalishaji nishati ya umeme.

Ahadi za Rais Kikwete hazijatekelezwa
NI vema wananchi wamemaliza mwaka 2011 na kuanza mwaka mpya wa 2012. Hata hivyo, ukweli utabaki palepale; wengi wao hawatasahau kauli tata na ahadi mithili ya Abunuwasi zilizotolewa na Rais wa Jamhuri, Jakaya Kikwete.

Kikwete kamlisha kasa Jaji Damian Lubuva
HIVI karibuni, Rais Jakaya Kikwete, alimteua Jaji mstaafu Damian Lubuva kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Rais na serikali wanalidharau Bunge?
SAKATA la David Jairo linaelekea kusahaulika. Hii si bahati mbaya bali ni mpango mahsusi. Kwa bahati mbaya, mkakati wa kupunguza makali ya ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoshughulikia suala hili unafanana sana mikakati mingine ya huko nyuma.
Tunaikumbuka Richmond; kamati teule ilitoa ripoti na kusababisha baraza la mawaziri kujiuzuru na kuundwa upya.

Rais Kikwete atibua nyongo
- NISHANI ZA UHURU
RAIS Jakaya Kikwete ametunuku nishani 57 kwa alioita, “Watu waliotoa mchango mbalimbali ya kutukuka katika nchi kwenye miaka 50 ya uhuru wake. Nishati hizo ni ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwenge wa Uhuru daraja la kwanza na Mwenge wa uhuru daraja la pili.

Kikwete akaliwa kooni
- Naye atakiwa kujiuzulu
- Waraka mzito wavuja
- CHADEMA yaitwa ‘mchawi’
RAIS Jakaya Kikwete amekaliwa kooni. Wakati chama chake kinakabiliwa na wimbi la kukimbiwa na wanachama na viongozi, swahiba wake anashikilia kuwa wenye “tuhuma za ufisadi” wajiuzulu kama yeye.
Kikwete atavua magamba mangapi?
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), sasa kinatafuta mlango wa kutokea baada ya kushindwa kutekeleza kwa vitendo mradi wake wa kujivua gamba.
Ukweli wa kama kimeshindwa kujivua gamba uko wazi, kinachokosekana sasa ni ujasiri wa kukiri hadharani kuwa kimeshindwa.
Tangu kushindwa kutekeleza mradi huo, kumekuwa na kauli tofauti zinazotafuta kupunguza makali ya aibu ya kushindwa kutoka kwa viongozi wakuu wa chama hicho.
Kwa mfano, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, Wilson Mukama, katibu mkuu wa chama hicho, amenukuliwa akisema, “Sharti
CCM na urais wa makanisani
BAADA ya vikao vya Chama cha Mapinduzi vilivyomalizika mjini Dodoma wiki mbili zilizopita, taarifa ilitolewa na wasemaji wa chama hicho kuwa mojawapo ya matatizo yanayokikabili chama hicho ni minyukano inayotokana na mbio za kuusaka urais wa mwaka 2015.
Mapema mwaka huu, baadhi ya wanaohisiwa kuwa tayari wameanza harakati za kuusaka urais, waliitwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara, Pius Msekwa na kuonywa kuwa wasiendelee na harakati hizo.
Aidha, taarifa ya kamati ya wazee watatu walioteuliwa na chama kutafuta suluhu ya minyukano ndani ya chama – rais msta

JK kweli rais wa CCM
NIMEWAHI kuandika katika safu hii kauli nzito ya kwanza aliyotoa Barack Obama baada ya kushinda urais nchini Marekani.
Alisema, “Mimi ni rais wa Wamarekani.

Kikwete, Lowassa hapatoshi
HATIMAYE Edward Lowassa ametoka hadharani na kuonyesha kuwa anataka kupimana ubavu na Rais Jakaya Kikwete.
CHADEMA yatikisa Ikulu
RAIS Jakaya Kikwete hakufahamu kwa undani kilichomo kwenye muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba (Constitutional Review Bill 2011), uliopitishwa na bunge hivi karibuni, MwanaHALISI limeelezwa.

CCM watamtosa Kikwete
KABLA ya kufikia uamuzi wa jambo fulani la kitaalam, wasomi hubungua bongo taaluma iwaongoze. Hakuna kupiga kura.
Kura hutumika katika masuala ya kisiasa. Mtindo huu wa kura huwa hauzingatii uzito wa hoja ila wingi wa kura kurahisisha mambo.
Upande unaopata kura chache huhesabika umeshindwa hata kama una hoja zenye maslahi.
Kikwete mtuhumiwa, tufanye nini?
UKURASA mpya kuhusu sakata la Richmond, umefunguliwa baada ya mambo mawili kutokea katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vilivyomalizika mjini Dodoma Alhamisi iliyopita.

Namhurumia rais wangu Kikwete
WIKI iliyopita ilikuwa mbaya sana kwa rais wangu, Jakaya Mrisho Kikwete, kwa namna alivyoumbuliwa mkutanoni na rafiki yake, Luteni wa Jeshi Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa, ambaye tumeambiwa mara nyingi kuwa hawakukutana barabarani.
Katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Dodoma , Lowassa alipewa dakika saba tu kusema jambo naye akazitumia vilivyo, kwa kifupi na kwa ufasaha.
Nimeambiwa na wale waliokuwapo Dodoma , ndugu zangu wa Mwananchi, kama walivyoripoti katika gazeti lao, kwamba Lowassa alisema:
“Mwenyekit

Ikulu aibu tupu
VIGOGO kadhaa waandamizi serikalini na katika bunge wamenufaika na mamilioni ya shilingi yaliyokusanywa kinyume cha taratibu na David Jairo, katibu mkuu wizara ya nishati na madini, MwanaHALISI limeelezwa.

Gamba lamponza Kikwete
MRADI wa kujivua gamba umeanza kumyumbisha Rais Jakaya Kikwete. Baadhi ya marafiki zake tayari wamegawanyika; wengine wameanza kukata tamaa na wengine wanajisalimisha kwa wanaotuhumiwa ufisadi, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Dk. Slaa, Kikwete uso kwa uso
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakusudia kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa umma, iwapo atagoma kukutana nao, imeleezwa.

Mzigo wa makundi wamuelemea Kikwete
KILE kinachoitwa, “Utafutaji tiba ya makundi” yanayohasimiana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bado hakijapatikana.
Mikutano miwili iliyofanyika jijini Dar es Salaam na ule wa jijini Arusha, badala ya kumaliza mpasuko uliokuwapo, imeishia kupambanua makundi hayo.
Kwenye mkutano wa Dar es Salaam, uliofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, 31 Oktoba 2011, makundi mawili hasimu – lile linalodaiwa kubeba watuhumiwa wa ufisadi na lile linalojiita “wapambanaji ufisadi” – yalitumia vikao hivyo kujiimarisha na kuonyesha wapambe wao kwamba bado wako imara
Kikwete na Museveni wanaelewa ujumbe wa wasomi?
SIKU ya Kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tarehe 20 Oktoba 2011, ilikuwa siku ya msukosuko kwa watu wawili maarufu – Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Jakaya Kikwete.

Kikwete maji ya shingo
RAIS Jakaya Kikwete amebakiwa na njia mbili tu kulinda nafasi yake katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Nguza anasota, wauaji wanasamehewa
BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitia saini hati tatu za adhabu ya kifo katika kipindi chote cha uongozi wake. Hati mojawapo ilikuwa dhidi ya Said Mwamwindi ambaye mwaka 1972 aliua kwa kumpiga risasi aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Dk. Wilbert Kleruu.

Rais Kikwete anazungumzia Tanzania ipi?
RAIS wetu, Jakaya Kikwete alituhutubia Watanzania na kutueleza mengi juu ya ya mafanikio aliyoyapata hivi karibuni katika safari yake ya ughaibuni huko Marekani. Huko pia alipata fursa ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Ahadi za Kikwete ‘bomu’
AHADI kadhaa ambazo Rais Jakaya Kikwete alitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, sasa imethibitika haziwezi kutekelezeka, MwanaHALISI limeelezwa.

Rais Jakaya Kikwete dhaifu?
- Ni taarifa za WikiLeaks
- Adaiwa kumuogopa CDF
RAIS Jakaya Kikwete amezidi kuandamwa. Sasa anaitwa “dhaifu na anayetishwa na wasaidizi wake.”
Mtandao wa WikiLeaks unaoibua taarifa za siri za kibalozi duniani, umeandika kuwa Rais Kikwete aliwahi kumwogopa mkuu wake wa majeshi, Jenerali Mwita Waitara.

Rais Jakaya Kikwete aanikwa
MAISHA binafsi ya Rais Jakaya Kikwete, kabla na baada ya kuwa rais yameanza kuanikwa duniani kote kwa njia ya mtandao ambako anatuhumiwa hata “kupewa zawadi ya suti” na fedha taslimu.
Tuendelee kumwamini JK?
NIMEKUWA nikijiuliza maswali kadhaa kichwani na moja ya maswali hayo ni, “Je, tuendelee kumwamini Rais Jakaya Kikwete au inatosha?”

Kikwete amepasua jipu la udini
IDADI kubwa ya wasomaji wanapata mawazo mbadala juu ya mwelekeo wa nchi, zaidi kupitia kwenye magazeti yanayofanya uchunguzi kuibua uozo, wizi, ubadhirifu au ufujaji wa mali na raslimali za nchi na ukiukwaji wa sheria za nchi na utawala bora.

Rais Kikwete chupuchupu
RAIS Jakaya Kikwete amenusurika kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, taarifa za ndani ya Bunge zimeeleza.