Slaa
Mlolongo wa Habari zinazomhusu Wilibroad Slaa

‘JK anavunja Katiba’
DK. Willibrod Slaa amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda.

Dk. Slaa, Kikwete uso kwa uso
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakusudia kumshitaki Rais Jakaya Kikwete kwa umma, iwapo atagoma kukutana nao, imeleezwa.

Dk. Slaa: Serikali haiaminiki
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amesema serikali ya Rais Jakaya Kikwete haiaminiki tena machoni mwa wananchi na jumuiya ya kimataifa.

Matatizo mengine CHADEMA mnajitakia
UCHAGUZI mkuu wa kuchagua viongozi wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) umekuja na mambo yake. Mengine yalitarajiwa na mengine hayakutarajiwa.

Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete
- Amtaja tena katika ufisadi
- Avuruga mkakati wa “gamba”
TUHUMA za ufisadi ambazo Dk. Willibrod Slaa amemshushia Rais Jakaya Kikwete, zimezima mbwembwe na majigambo ya “mapambano dhidi ya ufisadi” ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), MwanaHALISI limeelezwa.

Dk. Slaa: Kikwete ahadaa wananchi
MUSWADA wa serikali wa “Sheria ya Marejeo ya Katiba” wa Mwaka 2011, umeelezwa kuwa ni kitanzi kwa wananchi.

Uislam wa CCM na Ukiristo wa CHADEMA
NALAZIMIKA kuandika makala hii ili kutoa mchango wangu juu ya mjadala tete unaoendelezwa na viongozi wa dini na wanasiasa. Kwa kuwa imekuwa kawaida kwa watu kuzungumzia suala hili jumlajumla tu.

Slaa, Mwakyembe watishiwa kuuawa
- Membe, Mengi, Mwandosya nao wamo
- IJP: Tuna taarifa hizo, tunachunguza
- Sheikh Yahaya Hussein naye ahusishwa
KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini, Dk. Willibrod Slaa ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotishiwa kuuawa.

Wananchi wanalia, rais analia
KATIKA hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa Februari 2011, Rais Jakaya Kikwete alikiri kwamba hali ya maisha ni ngumu. Akajitetea, hata wakati wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere maisha yalikuwa magumu pia.

CCM: Mwisho wa nyakati?
AGOSTI mwaka 2006, akiwa hata hajatimiza mwaka mmoja madarakani, Rais Jakaya Kikwete alipata mmoja ya mitihani yake ya kwanza.

Kikwete aogopa ‘vyama vya msimu’
- Dk. Slaa: Tunafanya kazi ya kisiasa
RAIS Jakaya Kikwete, ambaye miezi mitatu iliyopita alisema vyama vya upinzani visichaguliwe kwa kuwa ni “vyama vya msimu,” sasa analalamika kuwa CHADEMA inataka kuangusha serikali yake.

Kelele za udini ni ghiliba za watawala
Tangu mwaka 1995 Dk. Willibrod Slaa alipochaguliwa katika mazingira magumu ya kisiasa kuwa mbunge wa Karatu, hakuna mtu aliyemwangalia kama Mkatoliki.

Unyama wa polisi Arusha na maigizo kwenye TV
MKANDA wa picha unaotumiwa na polisi kuonyesha kile ambacho inadai kilitokea Arusha, hauwezi kulibakizia heshima jeshi hilo.

Marando, Slaa wamvaa Kikwete
MWANASHERIA mashuhuri nchini na mwasisi wa mageuzi, Mabere Marando amesema, Rais Jakaya Kikwete hana nia njema ya kuleta katiba mpya, bali amejitumbukiza kuteka hoja ya katiba.

Urais wa Kikwete utata mtupu
MATOKEO ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa Oktoba mwaka huu, yanazidi kuzua utata, MwanaHALISI limeelezwa.

Dk. Slaa hekima imepita kiti cha enzi
MOJA ya makala niliyoandika mara baada ya uchaguzi mkuu, ilihusu kiongozi mmoja wa kale ambaye dini zote kubwa za Uyahudi, Uislamu na Ukristu zinamtambua kutokana na uongozi wake wa hekima.

Dk. Slaa: Tutamshitaki JK
RAIS Jakaya Kikwete anaweza kujiingiza katika mgogoro wa kisiasa na kidiplomasia, iwapo atashindwa kuchukua hatua za kuandika Katiba mpya na kuwa na tume huru ya uchaguzi, MwanaHALISI limeelezwa.

JK na kibarua kigumu
Miaka mitano iliyopita, tunaweza kuitafutia udhuru wowote ule kueleza kwa nini baadhi ya mambo hayakufanikiwa. Tunaweza kutafuta sababu ya kwanini baadhi ya mambo yalifanyika na mengine hayakufanyika kama ilivyotarajiwa.

Dk. Slaa: Uchaguzi wizi mtupu
MATOKEO ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yamejaa utata, MwanaHALISI limegundua.

Tanzania: Nchi moja, ma-rais wawili
JAKAYA Mrisho Kikwete amewataka waandishi wa habari kusaidia kuponya majeraha “yaliyotokana na uchaguzi mkuu.â€

CHADEMA: Matokeo yetu yamehujumiwa
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatuhumiwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani kwa lengo la kukinyima ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), MwanaHALISI imeelezwa.

Ya Nixon kuikumba Ikulu ya Dar?
SERIKALI haikutoa tamko kulaani au kusikitishwa na tukio lile, kampuni za simu za mkononi nazo zilikaa kimya, na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) haikuwa na jibu.
Lakini wote walitumiwa ujumbe kupitia kwenye simu uliobeba kashfa dhidi ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Salaa.
Ujumbe huo uliotumwa kupitia Na. +3588976578 na Na. +3588108226 ulisema Dk. Slaa ni “mropokaji†anayelumbana na vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi.

Kwanini nitampenda Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete ataweza kuingia katika historia, iwapo atahakikisha kipindi kilichobaki cha kampeni kinamalizika kwa amani.

JK katika mabango, Dk. Slaa mioyoni mwetu
SIJALI ni nani atakuwa Rais wa nchi hii kesho. Hiki si kitu kinachoninyima usingizi kuliko mwelekeo mzima wa upepo wa siasa ya nchi. Kinachonishangaza ni hicho hapo juu katika kichwa cha habari.

Dk. Slaa chaguo sahihi, kwa wakati sahihi
CHAMA kilichopo ikulu, kinatetemeka. Kinafikiri jinsi Dk. Willibrod Slaa atakavyoingia madarakani na kuunda serikali itakayoleta mabadiliko.

Wizi wa kura wanukia
MAWAKALA wa vyama vya siasa wanaosimamia uchaguzi, wametengewa “kiasi kikubwa†cha fedha ili kusaliti wagombea wao, MwanaHALISI limeelezwa.

Heri kwa watakaochagua mabadiliko
JUMAPILI hii, wananchi wataamua nani avuke mabonde na vichaka vyenye miiba ili aingie jumba kubwa, jeupe, la zamani, lililoko kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam – Ikulu.

Dk. Slaa aongoza kura za maoni
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa anaendelea kupeta katika kura za maoni zilizopigwa katika mitandao mbalimbali nchini, imefahamika.

Dk. Slaa: Mjenzi makini wa taifa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepata msaidizi mpya katika kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwezi huu.

Kila uchao ni mbinu chafu mpya, tuzipuuze
KWA muda wa wiki sasa nimekuwa natumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu zangu zikilenga kumkashifu mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.