Simba
Mlolongo wa Habari zinazohusu Klabu ya Simba
Ushindi wa mbeleko aibu Yanga, Simba
FUNUNU na malalamiko juu ya upangaji matokeo katika mechi za Ligi Kuu ya Bara huwa yanapuuzwa kwa madai ya kukosekana ushahidi. Klabu ndogo za soka zimekuwa zikilalamika kwamba Yanga na Simba zinabebwa, lakini hazisikilizwi.
Leo, hiki kilichotokea katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar kinathibitisha klabu hizo kongwe katika soka nchini zinabebwa. Wakati kila shabiki ameona na amesikia, waandaaji michuano wameamua kufumba macho.
Mashahidi ni makocha Salum Bausi wa Miembeni na Stewart Hall wa Azam FC, na kiongozi wa klabu ya Miembeni.

Visingizio basi, Simba kanyaga DC Mtema Pembe
HATA kabla ya kutia mguu uwanjani, Simba ya Dar es Salaam, ililalamikia hatua ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi yake dhidi ya Wydad Athletic Club (WAC) ya jijini Casablanca, Morocco.

Nyota ya Kaseja kung’ara tena Misri?
MASHABIKI wa soka wa jijini Cairo, Misri watakuwa na shauku ya kumwona tena Juma Kaseja Juma, kipa wa Simba aliyezuia mikwaju ya wapigajimahiri wa Zamalek katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba yapata bahati mara tatu
KLABU ya soka ya Simba ya Dar es Salaam imepata bahati nyingine. Bahati ya kwanza ni kurejeshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuafiki rufaa yake dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Yanga, Simba zakosa ‘minoti’ FIFA
KLABU 400 zilizotoa wachezaji walioshiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika zinatarajiwa kupata mgawo wa mapato ya mechi hizo.

Njia ya Simba kutwaa ubingwa hii hapa
- Yanga kuanza na Dedebit ya Ethiopia
MABINGWA wa soka nchini, Simba ya Dar es Salaam watapaswa kuvuka hatua tatu ili kuweka hai matumaini ya kufika robo fainali na hatimaye kutwaa ubingwa wa Afrika.

Asante Phiri, Papic
ASANTE kocha wa Simba Patric Phiri. Asante kocha wa Yanga Kostadin Papic kwa kutufundishia timu zetu zikaweza kucheza mpira nzuri wa kuvutia.

Kwa tamasha hili, Simba waa waa...
KWA mwanamichezo yeyote mwenye upeo, wazo la Klabu ya Simba ya kuanzisha siku maalumu ya klabu hiyo ambayo wameibatiza jina la 'Simba Day', linastahili pongezi.

Simba, Yanga na ushiriki wao kuiua Taifa Stars
MEI 3 mwaka huu, Shirikisho la Soka Misri (EFF), lilipitisha uamuzi wa kuzizuia klabu za nchi hiyo kusajili makipa kutoka nje ya nchi hiyo, kuanzia msimu ujao wa ligi.

Danny Mrwanda 'amefulia'?
TIMU ya soka ya Simba, kama zilivyo klabu nyingine zenye misuli ya kifedha, imefanya kufuru katika usajili, kwa kujaza nyota wa ndani na nje ya nchi.

TFF wanajua sababu za Yanga kususia
KLABU ya Yanga iliyoingia kwenye michuano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati kama timu ya pili iliyotokana na Tanzania Bara kuwa wenyeji wa michuano hiyo, inaambiwa imehujumu michuano.