Uchaguzi
Mlolongo wa Habari za Uchaguzi
JK bingwa wa kufanya kinyume
NAWASHUKURU wapenzi wasomaji wa safu hii kwa maoni yao. Baadhi walinipigia simu na wengine, kama ilivyo ada, walinitumia ujumbe mfupi wa simu.

Wabunge waliobebwa ni batili
WABUNGE 20 wamepita bila kupingwa. Miongoni mwao yumo waziri mkuu, Mizengo Pinda. Taarifa zinasema kupita kwa wabunge hawa kumetokana na kile kinachodaiwa, “Vyama vya upinzani kushindwa kusimamisha wagombea.”
Hata hivyo, jambo moja ni wazi: Kwamba katiba ya Jamhuri ya Muungano haitambui wabunge wa aina hii: Katiba inataja wabunge wa aina tatu tu – wale wa kuchaguliwa, kuteuliwa na mwanasheria mkuu wa serikali ambaye anaingia kwa wadhifa wake.

Bukoba watilia shaka ahadi za Kikwete
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete amedondosha ahadi Bukoba mjini kwa maratajio ya kuchota kura. Anatafuta kuendelea kupanga ikulu.

TEMCO washupalia serikali
“KAMA serikali inatenga kiasi cha Sh. 60 bilioni kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kuendesha uchaguzi, inatakiwa ifanye hivyo kwa kutenga angalau shilingi bilioni moja kwa ajili ya uangalizi.”

Kumbe CCM ni chui wa karatasi?
KWANZA alianza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, Julai mwaka huu, Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilipomuomba na kupendekeza Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, agombee urais.

Kinana anatekea maji kwenye pakacha, halijai
KAULI ya kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kwamba chama chake hakihusiki na ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeibua mengi.

Lugha moja, watu tofauti
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa na mwenzake wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba wanazungumza lugha inayofanana wakati huu wa kampeni.

Kiwewe kitupu CCM
KOMBORA lililorushwa na muasisi wa mageuzi nchini, wakili wa mahakama kuu, Mabere Marando limetia kiwewe Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya wasaidizi wake, MwanaHALISI limeelezwa.

Waziri Masha kaumbuka
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha, anadaiwa kusema uongo katika pingamizi lake kwa mgombea wa CHADEMA katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza.

Kikwete ana nini?
RAIS Jakaya Kikwete ameanguka mara tatu na zimetolewa sababu tatu tofauti zinazodaiwa kuchangia hali hiyo, MwanaHALISI limebaini.

Nimrod Mkono kupoteza ubunge
MBUNGE mteule wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ameingia katika kashfa ya rushwa ya uchaguzi na huenda akapoteza ubunge, MwanaHALISI limeezwa.
Hata Kikwete angehamia CHADEMA
RAIS Jakaya Kikwete amekuwa akijitolea mfano kila anapozungumzia suala la baadhi ya wagombea nafasi za urais, ubunge na udiwani majina yao kukatwa. Anasema wanatakiwa wavumilivu kama yeye.
Kwanza alijitolea mfano katika mkutano mkuu wa chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma baada ya kumteua na kumpitisha Dk Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais Zanzibar.
Pili alipochukua fomu ya kugombea urais mwaka huu na mara ya tatu alipozungumza na wafuasi wake katika ofisi ndogo za CCM, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, baada ya kurejesha fomu.

Dk. Slaa atibua CCM
MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema CCM haijawahi kuwa na ubunifu na uadilifu.
Najitoa mapema, sichagui CCM
MWAKA huu sitachagua mgombea urais, ubunge au udiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ninazo sababu:
Tunawatakia kampeni njema
KAMPENI za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba mwaka huu zinatarajiwa kuanza keshokutwa Ijumaa ambapo vyama vinavyoshiriki vitaanza kujitangaza.

CCM na dhambi ya uraia
MWAKA baada ya mwaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila kujijua kina utamaduni wa kujirudia katika madhambi yake.
Ntagazwa: CCM hii inatupeleka kubaya
ARCADO Ntagazwa, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), ameshtua watu baada ya kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Waliopita, waliobebwa kura za maoni CCM
HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepitisha wanachama 238 kugombea ubunge wa majimbo Tanzania Bara na Visiwani.

Kikwete aikosesha CCM jeuri ya mwaka 1995
MWAKA 1995 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa na jeuri. Baada ya mkutano mkuu kumteua Benjamin Mkapa kuwa mgombea urais wake, na Mwalimu Julius Nyerere akapita kumnadi, hofu ya kushindwa ilifutika.

Kazi ya Chama Vs Kazi ya Siasa
MWAKA 1903, ulitokea mgogoro mkubwa baina ya viongozi wawili wakubwa wa chama cha wafanyakazi nchini Urusi.

Wako wapi 114,630 wasipige kura
TAKWIMU za matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Zanzibar tarehe 31 Julai 2010 zinaonyesha kwamba watu 114,630 hwakujitokeza vituoni.
Kwa nini makapi wawe wakuu wa wilaya, mikoa?
MARA baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchukua fomu za kuwania kutetea kiti cha urais, alikwenda kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), mtaa wa Lumumba kuzungumza na wananchi.

Kauli za wananchi juu ya mgombea urais wa CHADEMA
Ufuatao ni mrejesho wa baadhi ya wasomaji 417 waliotutumia ‘sms’ juu ya mwandishi, maudhui ya makala na somo lenyewe – Dk. Willibrod Slaa.

Ushindi wa Dk. Slaa kuimarisha Bunge
- Mahasimu waweza kuwa upinzani
- Wakongwe waaga kwa msononeko
USHINDI wa Dk. Willibrod Slaa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, ndio pekee unaoweza kumaliza mivutano iliyokumba bunge lililopita, MwanaHALISI imebaini.

Tunataka mdahalo wa wagombea urais
KATIKA nchi zilizoendelea, jambo moja dogo linaweza kuharibu kabisa nafasi ya mgombea wa nafasi ya juu ya uongozi.

Makombora ya Dk. Slaa haya
UTEUZI wa Dk. Willibrod Slaa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano, "unamweka pabaya" Rais Jakaya Kikwete ambaye anatetea nafasi hiyo kwa muhula wa pili, MwanaHALISI limeelezwa.

CCM haiwezi bila rushwa
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba anasema hakuna tatizo la kushtua wakati huu wanachama wakishiriki kura za maoni za kutafuta wagombea. Anasema mambo ni shwari.

Msimu wa mashushu huu hapa
MSIMU wa mashushushu umewadia. Ni uzushi mtupu. Ni kupakazia. Ni utapeli uliokaangwa kwa mafuta masalia; chakula chake kina harufu sabini. Sasa mlaji ajue anakula nini?

Kura za maoni zimetufungua jinsi CCM inavyoasisi rushwa
ILI kuendelea kuishi viumbe hai wanategemeana. Kuanzia binadamu hadi wanyama wa mwituni, wanahitajiana ili maisha yawezekane.

Dk. Slaa kweli aweza kumshinda Kikwete?
JAWABU la swali hilo hapo juu linalobeba kichwa cha habari, kwa hakika, linategemea ni nani unamuuliza.