Dk. Slaa: Uchaguzi wizi mtupu

MATOKEO ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), yamejaa utata, MwanaHALISI limegundua.
Taarifa kutoka ndani ya NEC, vyama vya siasa na baadhi ya wagombea, zinasema matokeo yaliyotolewa yanatofautiana na kura halisi zilizopigwa.
Kwa mujibu wa baadhi ya mawakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), matokeo mikononi mwao yanatofautiana sana na yale yaliyotangazwa na Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).
Matokeo mikononi mwa mawakala kutoka mikoa 18 ya Tanzania Bara na mitatu ya Zanzibar, hadi juzi Jumatatu, yanathibitisha kuwepo tofauti kati ya idadi ya vituoni na ile iliyotangazwa na NEC.
Uchaguzi mkuu nchini ulifanyika Jumapili iliyopita kwa kuchagua madiwani, wabunge na rais, kwa upande wa Tanzania Bara na masheha, wawakilishi na rais Visiwani.
Katika jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, matokeo yaliyotangazwa na NEC yanaonyesha kuwa CCM imepata kura za urais 35,910, huku CHADEMA ikionyeshwa kupata kura 18,513.
Lakini matokeo ambayo yamekusanywa na mawakala wa CHADEMA yanaonyesha CCM imepata kura 20,120, huku CHADEMA ikipata kura 26,724.
Katika jimbo la Karatu, mkoani Arusha, hesabu za NEC zinaonyesha CCM imepata kura za urais 24,382, huku CHADEMA ikipata kura 41 tu; angalau kwa mujibu wa matangazo ya televisheni.
Bali kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa na mawakala na ambayo yamesainiwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi na msimamizi wa uchaguzi katika jimboni hilo, CCM imepata kura 24,364 na CHADEMA imepata kura 43, 137.
Jimbo jingine ambalo matokeo yake yamejaa utata ni Geita, mkoani Mwanza. Matokeo yaliyotangazwa na NEC katika jimbo hilo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 17,792, na CHADEMA imeambulia kura 3,989.
Lakini matokeo mikononi mwa mawakala yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 30,960 na CHADEMA kimepata kura 15, 736. NEC ilikiri kuwapo kwa kasoro katika jimbo la Geita na ilikubali kufanyia marekebisho.
Katika jimbo la Ubungo, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya NEC yameipa CCM kura 68,727 na CHADEMA kura 65,450.
Hata hivyo, kwa mujibu wa matokeo mikononi mwa mawakala katika jimbo hilo yanaonyesha kuwa CHADEMA imepata kura 72,252 na CCM kura 70,472.
Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya NEC kumtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi wa kiti cha urais.
Kwa mujibu wa NEC, Kikwete alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote halali zilizopigwa. Tume imesema kura zizopigwa zilikuwa 8,626,283.
Mshindani mkuu wa Kikwete, ambaye ni mgombea wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alitangazwa kuwa amepata kura 2,271,941 zilizo sawa na asilimia 26.34 ya kura zote halali zilizopigwa.
Katika mpangilio huo, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF alipewa kura 695,667 ambazo ni sawa na asilimia 8.06 ya kura zote halali.
Uchunguzi wa MwanaHALISI umebaini kuwa licha ya tofauti ya matokeo ya vituoni na yale ya NEC, matokeo katika baadhi ya maeneo hayakurekodiwa kwenye karatasi za tume, rasmi kwa shughuli hiyo.
Gazeti hili limeona matokeo yaliyorekodiwa kwenye karatasi za kawaida na magamba magumu ya makasha, ingawa zimegongwa mihuri inayoonekana kuwa ya tume.
Matokeo ya aina hii yanashurutisha kuwepo ujenzi wa shaka juu ya usalama wa kura na uwezekano wa matokeo kugushiwa.
Kwa mfano, katika jimbo la Segerea, mkoani Dar es Salaam, matokeo ya kura za urais yaliandikwa kwenye karatasi ya kawaida ya rangi ya khaki. Karatasi hiyo inaonyesha kuwa imetoka katika kituo Na. B – 2.
Katika kituo B – 4 ambako matokeo yameandikwa kwenye karatasi ya kawaida, CCM imepata kura 90 na CHADEMA kura 55.
Matokeo katika kituo hicho, kwa mujibu wa karatasi hiyo, yanaonyesha kuwa CCM imepata kura 94 na CHADEMA kura 90.
MwanaHALISI limeelezwa kuwa mbali na kasoro hiyo ya kutokuwapo kwa fomu za kurekodia matokeo, katika baadhi ya majimbo yaliyofanya uchaguzi, majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.
Gazeti hili lilitaka kujua maoni ya Dk. Slaa juu ya taarifa kuwa kuna maeneo ambako majumuisho ya kura za urais hayakufanyika.
Naye alijibu, “Wewe unazungumzia hilo; matatizo yaliyopo katika uchaguzi huu ni makubwa sana. Kuna uchafu mwingi. Ndiyo maana sisi tunasisitiza kuwa hatuwezi kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa.”
Amesema, “Tunaendelea kukusanya nyaraka zote za uchaguzi na si muda mrefu ujao, tutaeleza dunia ni kitu gani kilifanyika, wapi na akina nani walihusika. Tutaeleza pia hatua gani itakayofuata baada ya hapa.”
Gazeti lina taarifa kuwa baadhi ya majimbo ambako matokeo ya urais hayakutangazwa, ni Kiteto, Segerea, Muheza, Kibakwe, Kinondoni, Ilala na Moshi Vijijini.
“Huku kwetu hatukupewa nafasi ya kushuhudia zoezi la kuhesabu kura. Kazi hiyo ilifanywa na msimamizi wa uchaguzi ambaye alisema kura za rais zitahesabiwa wilayani,” anasema John Mrema ambaye aligombea ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia CHADEMA.
Anasema, “Lakini tulipofika katika ofisi ya mkurugenzi wa uchaguzi kule wilayani, tulimkuta msimamizi wa uchaguzi akiwa tayari na matokeo yake ya urais. Tulipomuuliza amepataje matokeo hayo wakati kura hazijajumlishwa, alikasirika na kuamua kuchana karatasi zote alizokuwa nazo.”
Akiongea kwa kujiamini, Mrema amesema, kwa ufahamu wake, mpaka sasa matokeo ya urais katika jimbo la Moshi Vijijini hayajatangazwa.
Mbali na kuwapo kwa kasoro za majumuisho, taarifa zinasema zaidi ya majimbo 25 yaliyoshiriki uchaguzi hayakuwa na fomu za matokeo Na. 21 (A) na 24 (A).
Aidha, masanduku 36 yaliyosheheni kura za urais, yalikutwa yamehifadhiwa katika shule binafsi ya Biafra iliyopo katika manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam.
Masanduku hayo yalikutwa yakiwa na karatasi zake halisi za kupigia kura na yalikuwa bado yamefungwa kwa lakiri. Katika orodha ya masanduku hayo kulikuwa na yale yaliyotolewa kwa Kata za Tandale, Makumbusho, Mwananyamala, Kigogo na Hananasif.
Kwa kata ya Tandale yalikuwa na namba: 162452, 162495, 1624586, 162489 na 162401. Makumbusho Na. 161330, Hananasif Na. 16871, 161051, 160958, 160165 na Kigogo Na. 160665.
Kutoka Morogoro, taarifa zinaeleza utata wa aina yake. Kati ya wapigakura 422 waliotarajiwa kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Msufini, kata ya Msufini, manispaa ya Morogoro, hakuna hata mmoja aliyekuwa na shahada ya kupigia kura.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434524.
Katika kituo cha Shule ya Msingi Misufini B – 2, Na. 00006226 kilichopo kata ya Mafinga, kati ya wapigakura 422 ni wapigakura 192 tu ambao walikuwa na sifa ya kupigakura. Hii ni kwa mujibu wa daftari la wapigakura PDF Na. 00434425.
Mbali na kasoro hizo, baadhi ya watu wanaonekana mara mbili katika daftari la wapigakura. Inaonyeshwa pia kuwa wana shahada mbili tofauti za kupigia kura.
Hapa ndipo zinachipuka taarifa zinazodai kuwa kwa kupitia majina hayo, na mengine ya ambao hawakujitokeza kupigakura, ulifanyika uchakachuaji matokeo.
Madai yamezagaa kuwa uchakachuaji kwa njia ya wale ambao hawakujitokeza kupiga kura, ama ulifanyika kupitia mawakala wa vyama vya siasa wasiowaaminifu au wasimamizi wa uchaguzi.
Katika jimbo la Babati Mjini pekee, yamekutwa majina zaidi ya 2,000 ya wapigakura wa aina hiyo. Miongoni mwao ni Ali Khera Sumaye ambaye amekutwa na shahada mbili.
Shahada ya kwanza ya Sumaye ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama cha NCCR- Mageuzi kabla ya kurejea CCM, ina Na. 12539414 na nyingine ni Na. 49947458. Taarifa nyingine zote za Sumaye, ikiwamo tarehe ya kuzaliwa zinafanana.
Shahada zote mbili zinamuonyesha Sumaye kuwa amezaliwa 17 Agosti 1952. Taarifa zake zinapatikana katika PDF Na. 00400518 ya daftari la kudumu la wapiga kura.
Naye Amina Abdallah Soono anatumia shahada Na. 1255139 na Na. 12557140; Anna Yakobo Masay, shahada Na. 1255831 na 12558205; Elinake Joseah, shahada Na. 26314248 na 49716656 na Jumapili Ramadhani Moromba mwenye shahada Na. 41226061.
Katika orodha hiyo, wapigakura wengine waliokutwa na shahada mbili ni Mariam Saidi Mohamed ambaye shahada zake ni Na. 12566932 na 49773838 na Ibrahim Richard Shalua Na. 32298659 na 12557313.
Taarifa za wapigakura hawa zinapatikana katika PDF, Na.004000518, Na.004000537 na Na. 00400534.
MwanaHALISI limegundua pia kwamba kuna baadhi ya wapigakura ambao majina yao yamekutwa katika daftari la wapigakura, lakini picha zao zinakosekana.
Haijaweza kufahamika iwapo wapigakura wanaoonyeshwa kuwa na shahada mbili walifanikiwa kupiga kura mara mbili au hata zaidi katika uchaguzi uliomalizika wiki iliyopita.
Lakini katika daftari la wapigakura kunaonyesha pia kuwa katika kituo cha Serikali ya Mt. Mbuyuni – 1 Na. 00006218, kata ya Mafisa, wapigakura 57 kati ya 410 hawakuwa na shahada za kupigia kura.
Miongoni mwa ambao hawakuwa na shahada ni Abas Ali Dunda, Abdallah Ali Matoto na Abas Majemba.
Mbali na kasoro hizo, MwanaHALISI limegundua mkanganyiko katika idadi ya walioandikishwa kupiga kura. Kwa mfano, Mkurugenzi wa NEC, Rajabu Kilavu alinukuliwa akisema tume yake imeandikisha jumla ya watu 21,210,187.
Hata hivyo, idadi hiyo ilipungua hadi kufikia wapigakura 19,686,608. Lakini Mwenyekiti wa Tume, Jaji mstaafu Lewis Makame alisema tume yake iliandikisha wapigakura 20,137,303.
Aidha, imefahamika kuwa timu ya wataalamu wa teknoljia ya habari (IT) ya CHADEMA ilitembelea mtambo wa kupokea matokeo ya uchaguzi siku mbili kabla ya uchaguzi.
Katika ziara hiyo, wataalamu hao waligundua kuwa mtambo huo haukuwa umejaribiwa kwa ajili ya kazi iliyokusudiwa.
“Tulipowaeleza kwamba ni makosa kitaalamu kutojaribu mtambo kama huu, ndipo walipoamua kuujaribu; na mara baada ya kuujaribu, ulikwama palepale,” anaeleza Mashinda Mtei, mmoja wa wataalamu wa CHADEMA waliokwenda kukagua mtambo wa NEC.
Anasema wakati wanafanya majaribio waligundua kuwapo kwa kasoro kubwa ya kura za mgombea mmoja kuhamia kwa mgombea mwingine.
Mara baada ya kugundua kasoro hizo, anaeleza Mtei, NEC waliahidi kurejesha Dar es Salaam kompyuta zote zilizokuwa zimesambazwa mikoani na kwamba waliahidi kufanya kazi hiyo na kuikamilisha haraka.
Tume iliahidi kuifahamisha CHADEMA juu ya maendeleo kuhusu kompyuta hizo.
Hata hivyo, katika hali ambayo haijaeleweka, siku hiyohiyo, tarehe 28 Oktoba 2010, Kiravu alimuandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA akikiri kuwapo kwa ujumbe wake katika ofisi za NEC.
Barua ya NEC yenye Kumb. Na. EA.75/162/08/99 ya tarehe 28 Oktoba inasema, “Napenda kukujulisha kwamba jana tarehe 27/10/2010, wataalam wa chama chako wa IT walikuja na kuruhusiwa kukagua mfumo wa kujumlisha kura.
Wataalamu hao waliridhika na mfumo huo na ni matumaini yangu kwamba wamekupatia taarifa kamili.”
Barua ya Kiravu ilipokelewa CHADEMA terehe 4 Novemba 2010, siku sita baada ya uchaguzi kumalizika.
Gazeti hili ambalo linaendelea kutunga taarifa za uchaguzi kwa makini zaidi, limeshindwa kumpata Kiravu kueleza mapungufu haya na kwa nini barua kutoka NEC kwenda CHADEMA ilichukua zaidi ya siku tano kuwafikia.
Wakati NEC ikisema wataalamu wa IT waliotumwa na CHADEMA wameridhika na mfumo wa kuhesabia kura, taarifa kutoka ndani ya chama hicho na ambazo zimethibitishwa na Dk. Slaa zinasema wataalamu wake waliupinga mfumo huo kwa maelezo kwamba haufahamiki kwa watendaji wa NEC.
Anasema kuthibitisha kwamba watalaamu wa chama walikuwa sahihi, zoezi la kuhesabu kura za rais na hata kumjulisha kura za wabunge ili kupata idadi ya wabunge wa viti maalum, limechukua zaidi ya wiki moja.
ni kweli kabisa kuwa huo ni uwizi na sasa watanzania lazima tuangalie bwana mkubwa kasema eti tunahuwisha katiba huo n uwizi mtupu kwani watanzania tunataka katiba mpya kwani jaji nyalali si alitoa mapendekezo vipi na yale ya jaji kisanga tunataka tena kamati za nini?now ni new constution na hiyo kamati isiwen ya wapenda kuvutia kwao
Jaman mi naona hi tz imeoza kwa sasa, kwanz jk na makamba ndo miozo no one, naamini tulikuwa tunafuatilia campaing, kitendo cha rais kusimamisha watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi kugombea, kilinisikitisha sana, kwan raia wa kawaida tu akiwa mahabusu bila kujua kama ana kosa au la, ikipata tatizo kwa familia yake haezi kwenda home iwaje wao? nahuzunika sana swala lamh sita la rais kupewa shinikizo binafsi achilia mbali uchakachuliwaji wa kura. jaman watanzania tunapelekwa wap? kama mafisadi ndio wanapewa kipaumbele? nan atutetee? watanzania tuamke tuache kudanganywa na aman huku tukikandamizwa, kwan amani inalindwa na mafisadi au wananch? Wao ndo wanataka kutuvuruga na kigezo chao cha udini, inamaana kura za urais alishinda kwa kupigiwa kura na waoslam? acheni kutuvuruga, na hakika mwisho umefika.
Hongera za pekee Kaka Kubenea, nimefuatilia angalau mwishoni mwishoni majadiliano kwenye SRAR TV asubuhi ya leo na kuvutiwa na hoja yako ya kushindwa kuamini madai ya udini katika kampeni na hatimaye uchaguzi mkuu uliopita.Wachunguzi wa mambo tunajua kuwa madai ya kuwa kuna ufa wa kidini ni mlango wa kuipitisha mahakama ya kadhi na OIC kama majibu kwa kisingizio hicho, na kwa kweli kama shukrani kwa kufanikisha mpango wa propaganda kali iliyopita. Ahadi ya kufanikisha hilo zimeanza kutolewa na watu wazito tu, zinazodaiwa siasa za kidini ni kiini macho cha kutupa lawama pasipohitaji kulaumiwa.Tuleteeni watanzania maendeleo msituletee migogoro na mabalaa! Tekeleza ahadi zako baba
Ama kweli mwennye ganzi hasikii moto;
Nashangaa sana Selikari na nchi yetu bado inatolewa macho na mafisadi,Kikwete hivi, mahakama siku hizi inashugulika na waharifu wa aina gani kama mafisadi makubwa kama hayo hayashughulikiwi na mahakama? au hiyo ndiyo maana ya maisha bora kwa kila TZ? Pili Ndug. Kikwete unapochukua fulsa ya kuongelea juu ya OAC ndanni ya selikari huoni unaleta udini ndani ya nchi yetu wakati katiba haizungumzii taratibu za dini?
chadema hongereni kwa kutoka nje...Mko juu .. lkn kumbukeni punda haendi mpaka apate fimbo.ss fimbo ya ccm ni chadema!!!! watakaa sawa tukiwa na katiba mpya..Usione wanajaribu kubeza kwa kitendo cha chadema kutoka nje ni kwasabababu wanajua wako madarakani kwa maslahi binafsi..Tuchape kazi UTAIFA MBELEEEEE
DAIMA ...Mungu anajua dhamiri zenu awabariki sana na awalinde ili mpambane mpaka kieleweke.
Hakika mimi nashindwa kuelewa huu udini ambao kikwete anausema umetokea wapi!kama ni udini basi umeonekana wazi kwenye awani yake ya nne coz hata uteuzi wake umeonyesha hivyo.asilimia 80%waisklamu 20%wakristu.jaribu kuangalia wakuu wa wilaya na mikoa utaona.Anyway watanzania wote ni ndugu ngoja niseme wanafaa niache kufikiria dini zao.lkn mimi naamini tatizo limeanza pale ambapo ccm wameiba kula na kikwete aache kuhusisha kudai haki kwa chadema na udini.wanachodai wabunge wa chadema ni haki CCM na tume ya uchaguzi waliiba kula.kibaya zaidi rais anatoa maneno ya kejeri kwamba wameenda watarudi yeye ndo rais wao mimi nilitegemea kwamba atatafuta suluhisho lkn kumbe ni mbinafsi kitendo cha kusema hivyo kinamaana ya udikteta na inabidi akumbuke chadema kina mamillion ya watanzania na kauli yake inaweza sababisha shida!Sidhani kama kikwete ana dhamila ya dhati na nchi hii!!!1
Ndugu yangu nakuunga mkono kuhusu maoni na mtazamo wako. Wale wakazi wa Dar wanaopenda kusikiliza redio hapana shaka watakubaliana nami kuhusu kampeni za kidini za wazi zilizokuwa zikifanywa na vituo vya dini za kiislamu. Gia aliyoiweka anashindwa kuiondoa na badala yake anakifukuza kivuli chake mwenyewe kwa kuomba watu wengine wakemee. Yeye ni Rais kwa nini asibainishe ni akina nani wanafanya siasa za udini? Kwa nini hapati ujasiri huo? KUMBUKA DHAMIRA DHALIMU HAIHITAJI HAKIMU! Ushauri wa bure Mzee wangu acha kugusia agenda hiyo kwani mwisho wa siku watu watagundua janja hii!
TANZANIA INAZIDI KUHOZA KWANI NYERERE ALISEMA CCM INANUKA IMEHOZA...KITU KILICHOHOZA HAKIWEZI KUWA NA UHAI TENA LABDA BWANA YESU AKIFUFUE KAMA ALIVYOFANYA KWA LAZARO...NANI ALIIFUFUA CCM..KWA SABABU HIYO TZ ITAENDELEA KUHOZA NA KUNUKA VIBAYA KWA MAANA INATAWALIWA NA CHAMA KILICHOHOZA...SIMIMI ILA NI KUTOKANA NA KAULI YA NYERERE.
KIKWETE HAYUMO MIOYONI MWA WATANZANIA TENA WAMEMCHOKA ILA AMELAZIMISHA TU...NA WATANZANIA HAWAIPENDI TENA CCM
SIKUBALIANI NA MAWAZO YA NYERERE NA YAKO CCM KUNA MATATIZO LAKINI BADO NDIO CHAMA PEKEE AMBACHO KINA MWELEO WA KULINDA AMANI UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA..WENGINE NI VYAMA VYA MSIMU.MUTAKUMBUKA MWAKA 1995 NYERERE ALISHIRIKI KW NGUVU ZAKE ZOTE KUMBEBA MKAPA, WASTAAFU WOTE KUANZIA KAWAWA,SALIM AHMED,MWINYI,POLICE JESHI NA USALAMA.NA WAKATI HUO CCM HAIKUWA TAYARI KUONA UPINZANI..LAKINI AUGUSTUINE LYATONGA MREMA ALIWEZA KUICHACHAFYA CCM NA KUPATA 27% YA KURA ZOTE...ZAIDI YA ALIZOPATA SLAA 2010. JEE CCM ILITAKA KUFA MIKONONI MWA NYERERE? JEE CCM WATANZANIA WALIOCHOKA CCM ? HAPANA MWAKA 2000 MKAPA ALIWASAMBARATISHA WAPINZANI KWA MBALI....SASA HAYA NI MAMBO YA MSIMU...WEWE ANGALIA KIKWETE AMEZUNGUKA NCHI NZIMA PEKE YAKE YEYE NA MKE WAKE NA AMEWEZA KUSHINDA ?
PILI LAITI WATU WANGEJITOKEZA KUPIGA KURA KWA WINGI BASI ANGESHINDA KWA KISHINDO ZAIDI.
MPENI SIFA YAKE ...DHARAU KWAKE HAISADII UPINZANI HATA SIKU MOJA
Hi,Kwanza Nyerere kusema nchi bila ccm haowezekani ni kauli ya kidikteta maana anazarau uwezo wa watu anaweka uchama mbele.Huyo unaesema amezunguka na mkewe na mtoto wake kukampeni hana mbinu za kampeni haeshimu wenzie wala kuwaamini ndio maana kafanya kifamilia,Pamoja na hayo huyo jamaa amechakachua sana kura kwa kutumia hao wanausalama matokeo yaliyotangazwa sio yenyewe,mfano segerea,ubungo ,vunjo n.k.Mimi naamini mtu mjinga kuliko wote duniani ni yule anaekubali haki na ukweli vikifichwa.Dr Slaa kwa kulijua hilo hataki kukubali kitu chenye utata,hii nchi ni kubwa ndio maana ccm wanaiba sana wakiona wamezidiwa hoja wanasingizia udini na ukabila sasa yeye angekuwa sio mdini namba moja iweje mambo Nyerere aliyoyakataza miaka ya nyuma kama Mahakama ya kadhi na OIC yeye kwenye awamu yake anayaanzisha tena kama si kutafuta maslahi ya upande mmoja.Huyo Jamaa kwa mawazo yangu hastahili kuwa rais wa nchi bora Salim hamed Salim au Amani karume wangepewa hii nchi lakini huyo jamaa hafai anajua udini tu.
TAFADHALI USITOE JINA KWENYE HIYO COMMENT
TAFADHALI USITOE JINA KWENYE HIYO COMMENT
TAFADHALI USITOE JINA KWENYE HIYO COMMENT
Nawapongeza sana mwanahalisi, Ombi langu kwa Chadema ninaomba waweke mambo wazi sisi tunajua chadema Tumeshinda tujulisheni au pelekeni tume ya uchaguzi mahakamani dunia ijue ile KIVUITU STYLE ya Tanzania Ilivyofanya kazi.Mwisho Hongera Rais Wetu DR Wilbrod Peter Slaa Kwa Ushindi Ninajua Wanakuchelewesha tu Lakini Watanzania TUMEKUKUBALI Lazima Kitaeleweke.
kaka walitaka kukutoa macho sasa watakutoa roho kabisa
sasa mbona wanalalAMIKA TU HAWTUAMBII KWAMBA KWA MAKUSANYO HAYO CHADEMA wameshinda kwa asilimia ngapi. au wameshindwa klakini matokeo siyo sahihi kuweni specific mtupe data kuwa baada ya kukusanya nakala za mawakala wenu mmepata kura ngapi na Jk NGAPI SIYOP MNALALMIKA WAKATI HAMTUPI MATOKEO YA JUMLA. SWALI MMESHINDA AU MMESHIDWA na je MAJIMBO 22 NI KIGEZO CHA USHINDI......... mbona CUF WANA 24 LAKINI WAMEKUBALI. ASIYEKUBALI KUSHINDWA......
SASA NAJIULIZA ZILE AHADI ZA KIKWETE ZAIDI YA MIA , AMESHAANZA KUZITEKELEZA HUKO? CCM IKO ICU SASA UNATEGEMEA ITARUDI WODINI 2015? IT IS A BIG NO.. YANI HURUMA TU, MKAPA ANA JAZBA HAYA JK NDIO KUCHEKA TU. NIMEKUWA NAFUATILIA BUNGE LA UINGEREZA, YANI SHUTUMA YOYOTE ILE INAYOIKUMBA SERIKALI LAZIMA PRIME MINISTER AINGILIE KUWEKA NENO SASA HUKO KITUKO TU CHA JUZI CHENGE KUTAKA KUGOMBEA USPIKA, JK YUKO KIMYA TU ... MIMI NI MKWERE JAMANI LAKINI HUYU MKWERE MWENZANGU NASHINDWA KUMUELEWA MWENZENU...
MWANAHALISI NAWAPONGEZA SANA SANA, KAKA SAID NIPO NA WEWE. JAMANI MBONA WENZETU HAWA WAZUNGU WANAJALI SANA MATAIFA YAO.. KWANINI SISI TUKO HIVI? JK PLEASE CHUKUA WATU KAMA AKINA KUBENEA. ANGALIA MIFANO KAMA YA AKINA OBAMA WALICHOKIFANYA. WE JK HUTAKI KUKOSOLEWA SASA UTAFIKA WAPI? 2015BSIYO MBALI MH. RAIS 2010 NDIO INAISHIA HIVYO, UMEBAKIZA MIAKA MINNE TU AMBAYO NI MIDOGO SANA HATA MTOTO ANAKUWA BADO HAJATENGEMAA.... MKAPA ANACHOFURAHIA NI NINI? MTU ANA MIAKA MINNE TU YA KUJIBU MASHTAKA, YEYE ANADELAY TU KUKUMBANA NA SHERIA NDICHO NAKIONA... HIVI MTU MWENYE AKILI TIMAMU ATAFIKIRIA KWAMBA 2015 CCM ITACHUKUA? KAMA HII TU WATU WALITAPATAPA... KIKWETE AKIULIZWA MASWALI YA MSINGI ANAKUWA NA KIGUGUMIZI TUNA TUNA TUNA TUNA MPANGO NA MARE MARE MARE LAKINI KWENYE KUOMBA KURA ANAONGEA KWA MIPASHO HUKU AKISAKATA RHUMBA. JAMANI TZ VP?
MDAU, UK
CCM nashindwa kuielewa kabisa... hivi wana conscious kweli hawa yani mkapa na kikwete ni aibu ya taifa, waache tuliwaona wababe africa hii acha kabisa sasa hivi wako wapi? au wanawaangalia akina gaddafi, museveni... kuanzia mwenyekiti sijui katibu mkuu wa ccm wote akili zao sawa. mimi ningekuwa JK ningewateua akina kubenea na chadema katika nyadhifa mbalimbali.. yani mwanahalisi mko juu mno nawapongeza. yani ukitaka kujua uozo wa tanzania njoo hizi nchi za wenzetu, huwa najiuliza wazungu wamewekea nini kwenye ubongo wao?
mdau
UK
Hivi hawa CCM wanamdanganya nani kama si kujidanganya wenyewe?
kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Mwisho umekaribia sana. 2015 hatutakubali tena mchezo walioufanya hata kama hao maaskofu wakisema hakuna atakayewasikiliza.
mmh huko kwa maaskofu usiende ndg yangu, hawajasema unaanza, muogope Mungu