Dowans wakubuhu wizi


Saed Kubenea's picture

Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 January 2011

Printer-friendly versionSend to friend
Mitambo ya Dowans

VIGOGO ndani ya serikali wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuilipa inyemela mabilioni ya shilingi kampuni ya Dowans, kabla taratibu muhimu kuhitimishwa.

MwanaHALISI lina taarifa kuwa Dowans Tanzania Ltd., imewasilisha ankara zake Hazina, tayari kwa malipo kabla maamuzi kusajiliwa mahakama kuu.

Wakati taarifa hizo zikivuja, umetokea utata wa kampuni ipi hasa ya Dowans ilipwe, kwani kuna makampuni mawili yaliyojitokeza.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) ndiyo ilikuwa na mkataba na Tanesco kupitia kurithi mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Bali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya Biashara (ICC) wa 15 Novemba 2010, unaagiza Tanesco kulipa Sh.185 bilioni kwa makampuni yote mawili.

Makampuni hayo ni Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited.

Utata huo unaongezeka kwa vile wakati wote wa mgogoro wa Richmond na Dowans, hakukuwa na Dowans Tanzania Limited ambayo sasa imetinga katika maamuzi ya ICC.

Nayo kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica), hata hivyo iliwahi kutajwa na msajili wa makampuni nchini Costa Rica kuwa haijawahi kusajiliwa nchini humo.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans ni mradi wa vigogo watatu wakubwa ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema, mpango wa kulipa makampuni hayo unasukwa kwa ustadi mkubwa na watumishi wawili –mmoja kutoka wizara ya nishati na madini na mwingine ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).

Alipoulizwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuhusu njama za kutaka kulipa Dowans kinyemela alisema, “Hapa ninapozungumza na wewe niko Kilosa. Sina taarifa za karibuni za ofisini.” Mkullo alikana pia kujua iwapo Dowans wamewasilisha ankara kwa ajili ya malipo.

Kwa mujibu wa sheria za usuluhishi nchini na zile za kimataifa, uamuzi wa ICC sharti usajiliwe katika mahakama kuu ya Tanzania.

Aidha, kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo katika mkataba kati ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Tanesco, yote yaliyokubaliwa ndani ya mkataba yatafuata sheria za Tanzania.

Hata hivyo, taarifa zinasema, msukumo wa kutaka malipo hayo kufanywa kinyemela, umefuatia kutajwa katika mwenendo wa kesi, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

“Hapa kuna kitu kinafichwa. Rostam hataki kesi hii isajiliwe hapa, maana jina lake limetajwa ndani ya kesi hii zaidi ya mara tatu. Hivyo anajua kuwa iwapo itasajiliwa ataumbuka,” ameeleza ofisa mmoja wa serikali.

Naye mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amethibitisha kuwa ankara za madai ya Dowans tayari zimewasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.

“Bodi ya Tanesco iliarifiwa jambo hili katika kikao chake kilichofanyika 21 Desemba 2010, na kila mmoja alishtuka,” ameeleza mtoa taarifa.

Alisema, “…wanaleta ankara za  madai hata kabla mahakama kuu haijasajili kesi yao? Hapana! Tukasema, sisi bodi hatuwezi kuidhinisha malipo haya…”

Kutajwa kwa Rostam katika shauri la Dowans kulifuatia kubanwa na majaji wa mahakama hiyo, mfanyakazi wake mmoja kutoka kampuni ya Caspian.

Mfanyakazi huyo aliyekuwa anahudhuria bila kukosa vikao vyote vya mahakama vilivyokuwa vikifanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alieleza mahakama, “…niko hapa kufuatilia maslahi ya bosi wangu.”

Mtoa taarifa anasema, “Yule bwana aliulizwa na wale majaji, mbona kila siku anaingia mahakamani na hatoki mpaka muda wa kesi unamalizika.”

Anasema, “Ndipo yule kijana akajibu, ‘nimetumwa na bosi wangukumwakilisha.’” Mahakama ikataka kujua huyo bosi ni nani? Ndipo akamtaja Rostam,” anaeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.

Anasema mara baada ya kutaja jina la Rostam, majaji waliokuwa wanasikiliza shauri lile, haraka wakauliza, ‘Kwani Rostam ni nani katika Dowans?’ Yule bwana akajibu, ‘Ni mwanahisa…’”

Kuna taarifa za kuaminika kuwa mmoja wa watu wawili waliosaini makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans, ni Henry Surtees, Mwingereza anayedaiwa kuwa mtumishi wa kampuni ya Rostam ya Caspian.

Wiki iliyopita, gazeti la kila siku la Mwananchi lilimnukuu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisema, Dowans ilisajiliwa nchini Costa Rica na Rostam ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria kusimamia malipo hayo.

Werema hakuzungumzia kwa undani hatua ya wanaojiita wamiliki wa Dowans kumpa Rostam nguvu hizo za kisheria.

Tarehe 7 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yoyote ya hisa kwenye kampuni mbili – Dowans na Richmond.

Mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans katika nyaraka za sasa zilizopo ofisi ya usajili wa makampuni (BRELA), Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amekana mara kadhaa kuifahamu kampuni hiyo.

Naye raia wa Canada, Andrew James Tice anayeonekana katika nyaraka za sasa za BRELA, aliwahi kuwa meneja uzalishaji katika kampuni ya Songas na baadaye kushika nafasi hiyo katika kampuni ya Richmond.

Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo gazeti linazo, Tanesco na Dowans wamekubaliana kuwa maamuzi yoyote ya suala hilo, ni lazima yafuate sheria za Tanzania.

Ibara ya 14 ya mkataba wao inasema pamoja na suala hilo kufikishwa ICC, pale ambapo kutatokea mgogoro, bado sheria za ndani ya Tanzania zitatumika wakati wa kufikia utatuzi.

Ibara ya 17 ya sheria ya usuluhishi inasema, mara baada ya maamuzi husika kutolewa, yatasajiliwa na mahakama kuu na baada ya hapo itachukuliwa kuwa ni amri halali ya mahakama ya nchi.

Nchini Costa Rica, ambako Dowans inadaiwa kusajiliwa, hakuna rekodi zozote inazoonyesha kuwapo kwa kampuni hiyo. “Dowans si kampuni halali ndani ya Costa Rica,” inasema barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini Costa Rica.

Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez, Jumamosi ya 3 Agosti 2008 na kutumwa ofisi ya katibu wa Bunge la Jamhuri, saa 11:09 jioni ya siku hiyo.

Mmoja wa wanasheria nchini ameliambia gazeti hili kuwa serikali haistahili kulipa hata shilingi kwa Dowans kwa kuwa kampuni hiyo ilinunua mkataba kutoka kwa kampuni feki – Richmond.

Amesema, “Hata hatua ya Dowans Holding kuingiza kampuni ya Dowans Tanzania Limited katika madai yao, wakati wakijua fika kwamba kampuni hiyo siyo iliyosaini hati ya kuhamisha mkataba, ni kinyume cha taratibu na sheria za makampuni.”

Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kutoka kampuni nyingine yenye utata ya Richmond ambayo ilipewa kazi ya kufua umeme kuanzia Januari 2007 hadi Juni 2008.

0
No votes yet
Soma zaidi kuhusu:

Tz we shld not involve On fight against government.we shld united and form a website tht will work on expose in each every details information of evil things that practice by government.that will set us free from hunger and haterage of our country. The aim of establish that site is to make them pay for what they have done evil things to our people.let them suffer as the way they make us suffer.its a time for tz to walking up and raise up with strong one voice on website.i prefer that website to be called by name of Newsleaks.com that site i want it to be very strong and powerful world wide.the use of this site is to expose the evils thing that practice by government to his own people without fear that hurts them .this site i want it not to work only on tz but to operate world wide.i want the world to realise that its time swept up mess and to stop practice evil thing to world.its a time for a man of peace to cut off of a chain of evil.and create a harmony world.

JK, ROSTAM, LOWASA, HAWA WATATU NDO CHIMBUKO LA HUU UCHAFU. NDIWO WAMEFUNGIA WATZ KONGWA ZITO KWA TAMAA YAO; ETI ROSTAM ANASEMA 185BIL NI KIPATO CHAKE CHA MIEZI 6??? YEYE NI MTU MAALUM SAN KTK TAALUMA GANI YA KUMTAJIRISHA HIVYO KAMA SI KUTOKANA NA KUTUMIWA NA HAWA MANYANG'AU? ADUI NA 1 WA TZ NI JK & COY ILA WATAKWEPAJE HUKUMU YA MUNGU WAO NI VIZAZI VYAO KWA DHULUMA WNAZOWATENDEA WATZ??? KILA SIRI ITATOKA, POLE SANA JK, HUTAFAIDI KITU. SI DINI INAKUFUNDISHA USIDHULUMU; MBONA UMEDHULUMU BILA AIBU?? SASA!?!?!

JK ANAJUA KILA UOZO NA NI YEYE ALIUBARIKI KWA TAMAA YA MADARAKA. KAMA 2005 ASINGEPATA ALIKUWA TAYARI KUUA; NA HATA SASA YUPO TAYARI KUUA KILA ANAYEPINGA UOZO WAKE. WA-TZ POLENI SANA HUYU NDO RAIS MLIYEMTUKUZA SANA. JK HAJAWAHI KUWA NA UWEZO NA KWA SASA AMECHANGANYIKIWA, NAWATAARIFU KWAMBA ATAJAKIMBIA NCHI AWAACHIE MKIUWANA. HUYU SI MWANADAMU.

Kuna haja ya Uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kulifuatilia kwa umakini suala hili. Aidha inaonyesha wazi kuna msukumo wa baadhi ya viongozi ni washiriki ktk sakata hili. Ni vyema viongozi wawe wazalendo ili tuweze kuinua uchumi wa Taifa letu la Tanzania.

Kuna haja ya Uongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kulifuatilia kwa umakini suala hili. Aidha inaonyesha wazi kuna msukumo wa baadhi ya viongozi ni washiriki ktk sakata hili. Ni vyema viongozi wawe wazalendo ili tuweze kuinua uchumi wa Taifa letu la Tanzania.

Thank you for a very informative article. I pray that all your
enemies perish immediately they attempt to frustrate your good efforts of informing the public. We are all behind you.

It has been difficult to believe even the person we trusted so much has turned ou to be the traitor(JK).

JK and those who side with him to betray our counrty deny the truth and they continue to compound their error by spending more to try and cover their sin that has already been uncovered and is now public knowledge.

Would like to remind JK and those behind him that "to deny the facts does not change the facts" figure it, they have been denying all allegations leveled against them, but with time they have been exposed to the full. And once they are through with the next five years of trying to cover up for their error, one thing is surely awaiting them..........HISTORY WILL JUDGE THEM HARSHLY

Thank you for a very informative article. I pray that all your
enemies perish immediately they attempt to frustrate your good efforts of informing the public. We are all behind you.

It has been difficult to believe even the person we trusted so much has turned ou to be the traitor(JK).

JK and those who side with him to betray our counrty deny the truth and they continue to compound their error by spending more to try and cover their sin that has already been uncovered and is now public knowledge.

Would like to remind JK and those behind him that "to deny the facts does not change the facts" figure it, they have been denying all allegations leveled against them, but with time they have been exposed to the full. And once they are through with the next five years of trying to cover up for their error, one thing is surely awaiting them..........HISTORY WILL JUDGE THEM HARSHLY

Kwa hali hii nchi haina sababu ya kuwa nchi ya amani na suluhisho la kuindoa CCM chama cha uangamifu wa watanzania masikini ni kuhamasisha mageuzi ya kuiondoa CCM madarakani

hi, brothers, i personally appreciate for what you are doing in the whole process of sensitizing the mass about what is going on concerning these two fake companies, Rostam and the like have put this country in mess where by only few people can stand up and shout loudly, thanks a lot because of have been there to make sure all of these are known by the poor tanzanian whom their resources and taxes have embezzled by few greed people from this piece of trush party called ccm. i urgue that you should continue with the same spirit though i know is not easy task but just remember that we are behind you and now we are ready to die for the liberation of this country. God bless you all and keepit up guys

safi sana kaka mmeweza kutuweka wazi yaliyokuwa yakifichwa.keep it up msiogope wala msitishwe.MASLAHI YA TAIFA MBELE....