FIDIA DOWANS: Wizi uleule, wezi walewale katika suti mpya

WATUHUMIWA wakuu wa ufisadi nchini wanashangilia. Waliojiita wapambanaji, wanazomewa. Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO), linajikuta lipo katikati na sasa linalazimika kutii agizo la mahakama.
Tarehe 15 Novemba 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), ilitoa amri kwa uongozi wa TANESCO kulipa fidia ya Sh.185 bilioni kwa kampuni ya ufuaji umeme ya Dowans Tanzania Limited.
Kampuni ya Dowans ilipata kazi hiyo baada ya kurithi mkataba wa kufua umeme kutoka kwa dada yake – Richmond Development Company (RDC), ambayo ilibainika baadaye kuwa haikuwa na hadhi, sifa wala uwezo wa kupewa kazi iliyoomba.
Hatua ya mahakama kuamuru TANESCO kulipa Dowans imefuatia uamuzi wa uongozi wa TANESCO kuvunja mkataba wake na Dowans.
Tangazo la kuvunja mkataba lilitolewa 30 Juni 2008 na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashid.
Taarifa zinasema, wakati Dk. Rashid anaamuru TANESCO kujiondoa katika mkataba wake na Dowans, mkataba huo ulibakisha siku 90 kumalizika.
Hivyo basi, wakati TANESCO ikikandamizwa na zigo la fidia; huku watuhumiwa wa ufisadi wakiendelea kupeta; na wapambanaji wakizibwa midomo; serikali inapaswa kueleza wananchi mambo mawili:
Kwanza, nani anayelipwa mabilioni yote haya ya shilingi za wananchi?
Anayetajwa kuwa “mmiliki” wa kampuni ya Dowans Holding Tanzania Limited, Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), amewahi kukana kumiliki kampuni hiyo.
Katika mahojiano yake na shirika moja la habari nchini Marekani, KLHN International, Machi mwaka jana, Bregedia Jenerali Al Adawi alisema, makampuni anayomiliki hayajishughulishi na mambo ya nishati bali ujenzi na kwamba Dowans siyo kampuni ya ujenzi.
Alisema iwapo kuna kampuni inatajwa kuwa yake wakati hajawekeza humo hata shilingi, basi angefurahi sana kupewa “kwa dezo” kampuni ya namna hiyo.
Mahojiano na Bregedia Jenerali Al Adawi yalifanywa na M.M. Mwanakijiji – mwandishi wa habari Mtanzania – anayeishi Detroit, Marekani.
Yalifuatia jina la Jenerali huyo kutajwa katika jarida la Africa, toleo la 7 Machi 2009.
Hii ilikuwa na maana kuwa Jenerali Al Adawi haifahamu Dowans na wala hajawekeza katika kampuni hiyo.
Lakini nyaraka mbalimbali za kampuni ya Dowans zilizopo kwa Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA), zinaonyesha Bregedia Jenerali Al Adawi kuwa mmoja wa wakurugenzi.
Anuani iliyotumika katika fomu hiyo ni P.O.Box 823, PC 112, Sultanate of Oman. Anuani hiyo ndiyo inayotumiwa na kampuni ya Services and Trade ya Oman ambayo Bregedia Jenerali Al Adawi alianzisha na mshirika wake mwingine mwaka 1977.
Sasa kama anayetajwa kuwa mmiliki wa Dowans anakana kampuni yake, nani anayelipwa fedha hizi?
Je, Bregedia Jenerali Al Adawi anaogopa nini kujitambulisha kuwa mmiliki wa kampuni hiyo?
Jibu ni moja: Kwamba kampuni ya Dowans Tanzania Limited, tayari waliudanganya ulimwengu wakati wa kuhuisha mkataba wa Richmond kwenda kwa Dowans.
Kwa muda mrefu wanaoitwa wamiliki wa kampuni hiyo wamekuwa wakitaja karibu makampuni manne ya Dowans ambayo walidai kuwa yanahusiana na Dowans Tanzania Limited.
Awali ilitajwa Dowans Holdings ya Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu. Lakini ghafla wahusika walibadilisha maelezo.
Hiyo ilikuwa baada ya taasisi ya Uwekezaji ya Dubai, Wizara ya Uchumi na Biashara ya Falme za Kiarabu ambayo hutoa leseni za biashara na Idara ya Kanda Huru za Falme za Kiarabu inayohusika na uwekezaji, kuthibitisha kuwa hakuna kampuni yenye jina hilo nchini humo.
Vilevile wamekuwa wakitaja kampuni ya Dowans Holdings ya Afrika Kusini. Lakini haikuchukua muda ilikuja kubainika, kwamba nchini Afrika Kusini hakuna kampuni yenye jina kama hilo ambayo inahusiana na Dowans Tanzania Limited.
Ilielezwa na wachunguzi wa habari kuwa herufi “SA” ambazo zinapatikana kwenye majina ya Dowans, zinasimama badala ya maneno ya Kiihispania “Sociedad Anónima” ambayo ni sawa na hadhi ya “shirika” katika Tanzania na siyo South Africa (Afrika Kusini).
Kampuni pekee ya Dowans ambayo ilionekana kuhusiana na Dowans Tanzania Limited ni ile ya Costa Rica.
Hata hati za madai zinathibitisha hili: Kwamba mbia mkuu wa Dowans Tanzania Limited, ni kampuni ya Dowans Holdings SA kutoka nchini Costa Rica.
Lakini ni katika nchi hii ambako sheria za uwekezaji zinaruhusu watu kufungua makampuni feki na zinalinda wawekezaji hao kutokujulikana.
Kwenye orodha ya wanaohusishwa na Dowans ni Kampuni ya Portek International ya Indonesia, kupitia kampuni yake tanzu ya Portek Systems and Equipment Ltd., inayodaiwa kuwa na hisa ya asilimia 39.
Sasa tatizo linaanzia hapa. Kwanza, kwa mwaka 2007 na 2008 kampuni hiyo ya Indonesia haikuwa na hisa yoyote kwenye Dowans Tanzania Limited wala haikuonesha kuwa wanaitambua kwa namna yoyote ile.
Pili, kwa upande wa Afrika, kampuni hiyo ya Portek Systems and Equipment ilikuwa inafanya kazi nchini Algeria kupitia kampuni ya Bejaia Mediterranean Terminals S.p.a. Portek, na kwamba ina asilimia 15 ya hisa kwenye kampuni moja tu ya kigeni nayo iko visiwa vya Philippines.
Sasa swali la kujiuliza ni hili: Kama haya ndiyo yaliyojificha nyuma ya pazia la Dowans, serikali inapata wapi mamlaka ya kulipa kampuni hiyo fedha za wananchi?
Kama anayejiita mmiliki wa Dowans Tanzania Limited na ambaye nyaraka za BRELA zinamtaja, Bregedia Jenerali Al Adawi kuwa ndiyo mwanzilishi, lakini mwenyewe anakana kumiliki kampuni hiyo, kwa nini TANESCO walazimishwe kulipa kampuni isiyofahamika wamiliki wake?
Kinachofahamika kwa wengi, ni kwamba Bregedia Jenerali Al Adawi ana sura nyingi: Anajitambulisha kama Mtanzania anayeishi katika nchi za Falme za Kiarabu.
Vilevile, Bregedia anajitambulisha kuwa mmiliki wa Dowans; huku anakana kuifahamu Dowans na kusema hajawahi kuwekeza katika kampuni yenye jina hilo.
Hapa ndipo inaibuka sura na tabia yenye utata. Hakuna hata anayejishughulisha kumhoji mfanyabiashara Rostam Aziz, ambaye aliruhusu anuani ya posta na barua pepe za kampuni yake ya Caspian Tanzania Limited, kutumiwa na Dowans.
Lakini kuna hili pia: Hatua ya serikali kunyamazia mkataba wenye utata na hata umiliki wa kampuni ya Dowans inafanana, kwa kiwango kikubwa, na umiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.
Kwa zaidi ya miaka sita sasa, serikali imeshikwa na kigugumizi cha kutaja mmiliki wa Kagoda. Wala haijasema sababu za kushindwa kumchukulia hatua mmiliki au kampuni yenyewe kwa kuchota zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Serikali inajua kuwa kati ya makampuni yote yaliyochota mabilioni ya shilingi kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT, Kagoda ndiyo ilikuwa kinara wa ukwapuaji huo.
Serikali inajua pia kwamba hata kabla Kagoda haijasiliwa, tayari ilishakwapua mabilioni hayo na kuyatawanya katika matawi saba tofauti ya benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Hivyo basi, ni muhimu kabla ya serikali kuamuru TANESCO kulipa “fidia”hiyo, kwanza itaje nani mmiliki wa Dowans, anaishi wapi na ameletwa na nani nchini.
Vinginevyo wananchi wataamini kuwa fedha zao zinakwenda kwa watu walewale walioshindwa kukamwatwa kwa zaidi ya miaka sita sasa tangu kutendwa kwa jinai.
Tatu, kabla ya serikali kuruhusu fedha kutoka kwa mlango wa nyuma, waliohusika kuingiza serikali katika mkataba huu wa kinyonyaji waonekane wakichukuliwa hatua.
Ni lazima serikali iseme, tena bila kutafuna maneno, kwamba wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria; na ionekane ikifanya hivyo.
Hatua ambazo zinasemwa, zisiishie kwenye majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari. Ziwe hatua zinazoambatana vitendo.
Nne, kabla ya serikali kukamua TANESCO, ambayo iko hoi kiuchumi, ieleze hatua ambazo itachukulia wanasheria wake waliokubali kuingizwa kwa kifungu cha kuruhusu mkataba kuhamishiwa kwa kampuni nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa, kuwapo kwa kifungu hicho ndiko kulikotoa mwanya kwa wamiliki wa kampuni ya Richmond kuhamishia mkataba wao kwa Dowans na hivyo kuifanya kampuni hiyo kuwa na kiburi hadi sasa.
Hivyo, kuwapo kwa kifungu hicho kuliipa haki Richmond kuhamisha mkataba wake na kufanya mkataba mzima kukosa maana, kwani dharula inafahamika kuwa ni muda maalum. Basi!
Wala wanasheria wa serikali hawawezi kujitetea kuwa hawakufahamu mkataba uliofungwa ulihusu uzalishaji umeme wa dharula. Walijua na wanajua mpaka sasa.
Kifungu hicho ndicho kinachodaiwa na baadhi ya wanasheria kuwa kilitumika kuingandamiza serikali katika shauri lililoamriwa katika mahakama ya kimataifa.
Tano, kabla ya serikali kulipa mabilioni haya ya shilingi, lazima iseme kipi kilimchochea Dk. Rashid kuamuru TANESCO kuvunja mkataba wakati uhai wa mkataba ulikuwa unaelekea ukingoni.
Je, nani alimsukuma Dk. Rashid kuchukua uamuzi huo unaoligharimu taifa hivi sasa? Wataalam wa sheria TANESCO hawakujua madhara? Je, wale wa serikali? Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuwepo kutoa maoni yake katika mikataba mikubwa ya aina hii? Je, wote walijia na kukaa kimya?
Kabla ya kuwa mtendaji mkuu wa TANESCO, Dk. Rashid alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Vodacom ambayo inajihusisha na biashara ya simu za mkononi.
Miongoni mwa wamiliki wa Vodacom alikuwa Rostam Aziz ambaye, amedaiwa kuwa mmiliki wa Dowans (ingawa amekana); swahiba wa Bregedia Jenerali Al Adawi na mfadhili wa Dowans kwa kuwaruhusu kutumia anwani za kampuni yake.
Sita, kabla ya kuamuru kulipwa fedha hizo, serikali inapaswa kuweka wazi ni hatua zipi itakazochukua dhidi ya Nazir Karamagi, ambaye wakati huo alikuwa waziri wa nishati na madini.
Ni Karamagi aliyekubalia Richmond kuhuisha mkataba wake kwa Dowans. Kosa la Karamagi hapa ni kukubali kuhuisha mkataba wa kampuni ambayo “haikuwapo kwa mujibu wa sheria.”
Huku akijua kwamba mkataba kati ya serikali na Richmond ulikuwa wa mwaka mmoja, Karamagi aliubadilisha na kuufanya kuwa wa miaka miwili.
Si hivyo tu; wakati Karamagi anasaini mkataba mpya, tayari janga kuu lililokuwa limesababisha serikali kuhaha kutafuta umeme wa dharula, lilikuwa limemalizika.
Saba, serikali iseme itamchukulia hatua gani aliyekuwa waziri wa nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha anayedaiwa “kushinikizwa” kuipa mkataba Richmond.
Hata kama Dk. Msabaha alishinikizwa, lakini ni wazi kuwa alishindwa kusimamia kazi za serikali kwa uaminifu alioapa kutunza; badala yake akaruhusu kampuni isiyo na hadhi kupewa mkataba.
Nane, kabla ya TANESCO kulipa mabilioni hayo ya shilingi, lazima serikali; na hapa Rais Jakaya Kikwete, aeleze atamchukulia hatua gani za kisheria, aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa kwa kuingiza taifa katika hasara hii ya mabilioni ya shilingi?
Kosa la Lowassa linafahamika. Anadaiwa kushikiza watendaji serikalini kuipa kazi kampuni isiyokuwa na sifa.
Kwa hiyo basi, hatua yoyote ya kulipa fedha bila kujulikana mmiliki halali, kutafanya wananchi waamini fedha zinalipwa kwa Kagoda yuleyule, lakini aliyekuja kupitia mgongo wa Dowans. Tusifike huko.
Katika jina la demokrasia na uwazi, serikali haina budi kutaja mmiliki wa Dowans Tanzania Limited na anakoishi wapi.
Ifahamike pia kampuni ilisajiliwa wapi na lini; nani wamiliki wake ndani na nje ya nchi; wabia wake ndani na nje; na hatua ambazo zitachukuliwa kwa watendaji wake.
Hadi hapa na sasa, hakuna uhalali wowote wa kulipa mabilioni ya shilingi za walipakodi wa Tanzania kwa vivuli vinavyoletwa kwa jina la Dowans. .
Tunaibiwa!
Kubenea, hakikisheni kazi zenu za kichunguzi kama hizi mnazifikisha kwa hao wanaoitwa nchi wahisani kwani hao wameonekana kuwa na sauti sana kwenye serikali zetu japo nao si wa kuaminiwa sana kwani nao wanafaidika na wizi wa raslimali zetu.
Hali ni mbaya sana kwani tuliotegemea kuwa watetezi wetu baadhi ndiyo wamekwisha jiuza kwa hawa wezi mf Zitto Kabwe.
kwa kweli inasikitisha sana na inashangaza sana na inafikia sehemu inabidi ucheke kwa uchungu mana kaka yangu Kubenea unajitahidi sana kupitia gazeti lako hili ambalo ni kinara wa taarifa za uchunguzi hapa Tz.lakini inaonekana ni bado watanzania hawajawa waelewa wa mambo hususan inapokuwa serikali haijatoa tamko basi huwa hawaamini hata uwaambie nini. Pia pamoja kelele zote hizo basi serikali itaendelea kulipa fedha hizo bila hata aibu ya maneno na malalamiko ya wananchi hio inatia uchungu sana. Kitu chengine ninavyofahamu kampuni kabla ya kupata usajili ni lazima vipatikane vitu viwili muhimu sana ambavyo ndani yake kunakuwa na mlolongo mzima wa kufahamu Jina la kampuni,wamilikina hisa zao,ofisi yake itakuwa wapi na lazima liwepo bango la kuashiria ilipo,shughuli zake zitakuwa ni zipi, shea zake zitakuwa zimegawanywa je, mipaka yake na majukumu yake, ama ni ltd kwa shea ama venginevyo katika muundo wake na mengine mengi. haya yote hupatikana kupitia "Articles & Memorandum of association" Hapo ndipo baada yakupitiwa na muhusika Registrar wa makampuni akiridhika nayo kampuni hiyo ina takiwa ilipie ada na kupatiwa usajili husika. Sasa tunapiga kelele kwani vitu hivyo havipo ofisini kwa muhusika? wa Tz kwa nini haviekwi hadharani? ili wa tz wakapata mwanga zaidi katika suala zima la nani hasa mwenyewe hio kampuni na hapo itafahamika ni Genuine au fake registered. pia tutafahamu kwa kiasi gani msajili kampuni alivyomakini au la. Kwa kifupi nimpongeze tena mwandishi wa habari hii pamoja n timu yake yote kuanzia wahariri hadi wasambazaji wake wote, wasichoke kutupa michapo kila wiki.
Sales & Marketing
F.A.Glass Work
Kwanza nikupongeze Kubenea na gazeti zima la mwanahalisi. Swadaktaa kabisa juu ya yote uliyoyahoji. Walijificha, sasa wanatokea wapi hao wamiliki? Kesi kufanyiwa nje ilikuwa njama ya kufanya mikakati ya kuiba??? Sasa kubwa kama mchango wangu ni kuwa:-
Najiuliza siku zote juu ya jambo hili kuchukua zaidi ya miaka mitatu linaongelewa na kupigiwa kelele kila kukicha. Hatujikiti kupambana na maendeleo ya nchi. Hivi Rais anafanya nini kiasi kwamba haoni shida juu ya hili. Yeye ni kama baba mwenye nyumba, ugomvi wa watoto kila siku hatoi karipio kwa aina ya kufichua ukweli wa jambo hili na kuchukua hatua?? Haoni aibu iliyoje kwa serikali yake kupakwa matope kwa kashfa za ufisadi?? Atapangua baraza la mawaziri hadi lini na je ataacha historia gani katika nchi yetu. Hakika "Dont judge a book by its cover"!! Kikwete aliingia madarakani mwaka 2005 huku watanzania tukiwa na mioyo yenye matumaini kuliko maelezo. Tulidiriki hata kumlaani Baba wa taifa kumpigia debe Mkapa 1995. Sasa Kikwete anaonekana si lolote si chochote kwa Mkapa. Aibu gani hii!! Kikwete toa kauli juu ya hili; ukilifumbia macho nawe utakuwa mmoja wao (Wafisidi wa rasilimali za nchi). Toa msimamo wako kupitia hotuba kwa wananchi za kila mwezi. Acha uzembe wa kuongelea misaada ya wamarekani wakati tunaendelea kulipatia hasara taifa letu. Acha Uswahili!!! Historia itakuhukumu!!! Waona Kenya?? Ok!!
uDINI mtupu !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
uDINI mtupu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Watanzania tufikie mahali tutangaze fatwa kuwa kichwa cha Rostam ni halali wakati wowote na kwa namna yoyote. Kama wake nyumba zake ndogo yaani Jakaya na Lowassa wataendelea kumkingia kifua nao tuwaingize kwenye fatwa hii.
Wako wapi wanajeshi wetu na watu wenye uchungu na taifa hili? Kwanini kuacha vita dhidi ya mafisadi kwa magazeti tu?
Wanyama wote ni halali isipokuwa mnyama mmoja mwenye sura ya binadamu aitwaye Rostam Aziz ambaye ni haramu kuliko hata nguruwe na ngamia. YAani amekosekana mtu mmoja jasiri akammiminia risasi? Hata matajiri wetu wanashindwa kutafuta watu wa kumfutilia mbali mbwa huyu hasa akiwa Dar es salaam, Dodoma hata kumfuata kwake Igunga?
Hivi huyu mwarabu ataendelea kututesa watanzania hadi lini? Watanzania amkeni kutoka kwenye usingizi. ifikie mahali tuseme sasa basi. Huyu rostam bado ametuweka utumwani kama Baba yake alivyowauza babu zetu kama njugu.
Mungu ibariki Tanzania
kubenea Mungu akujalie naamini watanzania tutazidi kukuombea ili uzidi kuwafumbua maana elimu ni ndogo mno ndio inayosababisha tuonekane hatujui mambo hasa inapofika kwenye swala la sheria. uchambuzi wako unaoesha unaipenda nchi yetu. Sisi tunakuombea endelea kuelimisha ili asilimia kuwa ijue nini kilifanyika na nini kifanyika kwa wakati gani. Na mimi nakuunga mkono kwa asilimia zote tujue na anamiliki, nani alisababisha taifa letu kupata hasara kubwa kiasi kama hiki. Pia je, kunahatua gani zilizochukuliwa ili hata walioko madarakani wajue siku wakifanya kosa mkono washeria utawakumba. Lakini kama tunafanya ubishoo ndani ya uchumi wetu na kunufaisha wachache huu ni wizi tena wajabu.
kubenea Mungu akujalie naamini watanzania tutazidi kukuombea ili uzidi kuwafumbua maana elimu ni ndogo mno ndio inayosababisha tuonekane hatujui mambo hasa inapofika kwenye swala la sheria. uchambuzi wako unaoesha unaipenda nchi yetu. Sisi tunakuombea endelea kuelimisha ili asilimia kuwa ijue nini kilifanyika na nini kifanyika kwa wakati gani. Na mimi nakuunga mkono kwa asilimia zote tujue na anamiliki, nani alisababisha taifa letu kupata hasara kubwa kiasi kama hiki. Pia je, kunahatua gani zilizochukuliwa ili hata walioko madarakani wajue siku wakifanya kosa mkono washeria utawakumba. Lakini kama tunafanya ubishoo ndani ya uchumi wetu na kunufaisha wachache huu ni wizi tena wajabu.
Ndugu Kubenea:
Huu ni mpango wa wizi wa mchana wala hakuna cha mahakama wala cha msuruhishi!!
ni mpango wa wizi
WIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIZI MTUPU
Sijui kwa nini hata TANESCO walienda kwenya mahakama hiyo wakati mmiliki wa DOWANS hajulikani
Hivi mahakama za kimataifa nazo pia zimeingiwa na wamafia? Haiingii akilini kuona kivuli kinashinda kesi! Hii inatokea Tanzania tu! Je pesa anapewa kivuli, endapo hapa kwetu hakuna kampuni/mtu aliyejityambulisha kuifahamu Dowans made in Tanzania & Costa Rica!
Poleni Watanzania tumeyataka wenyewe! Wakati wa uchaguzi tunachagua viongozi kama vipofu kisha baada ya uchaguzi tunalalama kama vichaa! Tulikwishatahadharishwa tuwe macho tuchague viongozi waadilifu. Kwa sababu ya ushabiki wa udini, tukachagua tukaendelea kuwaunga mkono mafisadi...Kwa sababu ya chumvi, kanga na kofia, wakachagua uozo...
Tuendelee tu kuteseka kwani inaonekana siasa za Tanzania zimekuwa kama ushabiki wa Yanga na Simba bila kujali uzalendo na masilahi ya taifa. Ufukara umekuwa ndio jadi yetu. Tunapiga miayo ya njaa kwa "amani na utulivu" wakati maghala ya nchi yamejaa kila aina za vyakula ambavyo vimekumbatiwa na vibaka wachache. Ni vema watanzania tuendelee tu kuteseka hadi tutakapopata akili!
Ni ukweli ulio wazi kuwa Tanzania hii inamilikiwa na wafanyabiashara(wezi) wawili ambao kwa kushirikiana na kibaraka wao wa tatu wako tayari kufanya chochote hata kama ni kuangamiza taifa hili ili mradi wapate faida, ni wajibu wetu sasa watz wote kwa pamoja kutake action cz wapiganaj wachache kama mwanahalisi c chochote kwa majambazi haya
Inasiktisha kuona serikali ikichezea fedha za walipa kodi na kuendelea kulifanya taifa na wananchi kuwa masikini..tunawaomba wanaharakati wote wapenda haki na wenye uzalendo wa kweli kutolifumbia macho hili..deni hili lisilipwe kabisa pia iundwe tume maalum ya kuweka mambo hadharani ili sheria ifuate mkondo wake...yaani ccm inanuka rushwa
Kubenea umemvua nguo Kikwete na wezi wenzake. Laiti watanzania wangekuwa wanayasoma haya kwa akili ya kawaida na kuyafanyia kazi. Hakuna haja ya kuteseke huku kina Rostam, Kikwete na Lowassa wakisaka pesa ya kuingiza jizi jingine ikulu mwaka 2015. Na tusipokuwa makini watafanikiwa. Wamefanikiwa kumuingiza spika wao ili kujenga mazingira ya kulinajisi bunge na kuhalalisha ujambazi huu. Mwanahalisi sina jinsi ya kuwapongeza kwa kujitoa mhanga kulinda hadhi na haki ya taifa letu. Bahati mbaya mko peke yenu. Kwani watanzania walio wengi ni kama kuku au tuseme kondoo. Wametekwa na genge la mafisadi la CCM hawafurukuti. Hapa wa kulaumu ni watanzania wenyewe kwa kujigeuza mbwa koko.
kila linalotokea tz watz tumekaa kulalama tu!!!!! nchi ishauzwa hii hapa wenye kauli watajilipa hata tufanye nini na tabia ya wabongo kuujificha nyuma ya kivuli cha uvunjifu wa amani isiyo kuwepo ndo chanzo cha mateso yote ya mtanzania..