Hatutaogopa vitisho


editor's picture

Na editor - Imechapwa 12 March 2008

Printer-friendly versionSend to friend
Maoni ya Mhariri

KWA mara nyingine, tumeendelea kupokea vitisho kutoka kwa watu tusiowafahamu, nia yao ikiwa ni kutuogopesha ili tuachane na utoaji taarifa kuhusu mafisadi.

Vitisho hivi havikuanza leo, ni muendelezo wa juhudi za mfa maji anayetapatapa. Mapema mwaka huu, baada ya kupokea vitisho kama hivi, watu hawa waliajiri wavamizi ambao waliendesha shambulio kwa Mkurugenzi Mtendaji Saed Kubenea na mshauri wa gazeti Ndimara Tegambwage.

Nia ya uvamizi haikuwa kudhuru mwili tu, bali walitaka roho za wenzetu hawa. Kwa habati mbaya kwao nia yao haikutimia, sasa wameanza tena vitisho.

Tunaomba kuwaeleza wasomaji wetu kwamba sisi hatuogopi vitisho hivi. Tunaendelea kuandika. Kuandika ndiyo kazi yetu tunayopenda, tuliyochagua na tuliyosomea.

Tunachukua fursa hii kuwashitaki kwa umma, wale walioshiriki uvamizi na wote wanaotoa vitisho kwa shabaha ya kutunyamazisha. Tuacheni tufanye kazi yetu.

Hatukusudii kumwonea mtu, wala hatutajiruhusu kutumiwa na watu kuendeleza visasi kwa nia ya kukomoana. Tutasimama katika maadili ya uandishi wa habari kwa kusema kweli daima.

Tusichotaka kufanya na ambacho hatutaki kushurutishwa kufanya, ni kuwa sehemu ya mtandao wa kufunika wahalifu, kusafisha maovu ya watu au kuwabeba watu wachafu mbele ya jamii.

Tutatoa habari na taarifa. Wananchi wenyewe, ambao ni waajiri wetu, watasoma na kuchukua msimamo kadri watakavyoelewa. Huo ndio uandishi tuliokuwa tukifanya; tunaofanya hivi sasa na tunaokusudia kuendelea kufanya. Tuwe pamoja.

0
No votes yet
Tangu Lowassa amwange pesa yake kwa Mwanahalisi hakuna kilichobakia bali nepi ya kumsafisha. Kwa wanaomjua Kubenea vizuri hawashangai badiliko hili. Maana ukiachia mbali kupata umaarufu si kwa umahiri wala uadilifu wake bali kumwagiwa tindikali kutokana na ukali na umahiri wa Ndimara Tegambwage, aliweza kuficha makucha yake. Kwa wanaomjua kama mchumia tumbo wa kawaida hawashangai badiliko hili la ghafla kutoka simba kwenda mbwa. Na bado mtamjua Kubenea ambaye hamkuwahi kumjua wala kumdhania. The guy is nothing but a goon who by accidentally landed on fame. Sitaki niongee mengi. Time will surely tell you and show you who Kubenea actually is.
nasema hivi hili gazeti limekwisha bora liondoke kabisa yani mwezi mzima gazeti lilelile. poleni sana
Sisi Wapenda Haki lazima tuwaunge Mkono
JJ