Kubenea awindwa


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 28 July 2010

Printer-friendly version
Saed Kubenea

MAISHA ya Mkurugenzi Mtendaji wa MwanaHALISI, Saed Kubenea yanaendelea kuwa hatarini.

Watu sita wakiwa na bunduki, walivamia nyumba aliyohama hivi karibuni, usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, mtaa wa Kitomondo, Temeke jijini Dar es Salaam na kulazimisha waliowakuta kuonyesha alipo Kubenea.

Baada ya kuambiwa amehama waliwaambia wako chini ya ulinzi; wakaanza kuwapiga na hatimaye kuwapora simu na fedha. Haikufahamika kiasi gani cha fedha kilichoporwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyera, amethibitisha tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi.

Hili ni tukio la pili baada ya shambulizi lililofanywa 5 Januari 2008, katika ofisi za gazeti hili, ambapo yeye na mshauri wa taaluma wa MwanaHALISI, Ndimara Tegambwage walijeruhiwa na kumwagiwa tindikali.

Hadi sasa, shauri linalohusu shambulio hilo bado linaendelea mahakamani, huku Kubenea akiendelea kupata matibabu ya macho mara kwa mara nchini India.

0
Your rating: None Average: 4 (1 vote)
Soma zaidi kuhusu: