Lowassa, Rostam kumzima Kikwete


Saed Kubenea's picture

Na Saed Kubenea - Imechapwa 08 June 2011

Printer-friendly versionSend to friend
Waahidi kumlipua vikaoni
CCM hatihati kuvunjika
Rostam Aziz

HATUA yoyote ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kuwafukuza ndani ya Chama Chaa Mapinduzi (CCM) wanaowaita “watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini,” yaweza kumuumiza mwenyewe, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya serikali na chama hicho zinasema watuhumiwa hao ambao Kikwete wiki mbili zilizopita waliitwa mbele ya makamu mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na kuhojiwa, wamejipanga kuzuia mpango huo na ikibidi watamgeuzia kibao kwa hoja kuwa yeye “ndiye tatizo kuu” katika chama na “chanzo cha serikali kuzorota.”

Wanaotakiwa kuondolewa kwenye uongozi ndani ya chama kwa hoja kwamba “wamechafua sura” ya chama hicho mbele ya wanachama na wananchi, ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge.

Lowassa anatuhumiwa kufanya upendeleo katika kuipa zabuni ya kuzalisha umeme kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (LLC), ambayo imethibitika kuwa haikuwa na uwezo, sifa wala fedha za kufanya kazi iliyoomba.

Rostam ametajwa mara kadhaa katika ufanikishaji wa mikataba tata ya kufua umeme ya Richmond/Dowans, pamoja na wizi wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd., katika akaunti ya madeni ya nje (EPA) iliyoko Benki Kuu ya Taifa (BoT).

Chenge, aliyelazimika kujiuzulu uwaziri, anatuhumiwa kuingiza nchi katika mikataba mbalimbali ya madini, ununuzi wa ndege ya rais na kujipatia mlungula katika ununuzi wa rada kama ilivyothibitishwa na shirika la uchunguzi wa makosa makubwa la Uingereza (SFO).

Mtoa habari wa gazeti hili ambaye yuko karibu na viongozi hao watatu anasema, “Lowassa, Rostam na Chenge wameapa kutoondoka CCM.” Anasema wameapa kukabiliana na yeyote anayetaka kuwaondoa.

Anasema, “Wewe unajua kwamba Rostam ametoa fedha nyingi sana kwa chama hiki. Sasa anasema wanaotaka aondoke lazima waseme aende wapi. Anasema lolote na liwe, lakini hakuna atakayejiuzulu wala atakayekubali kufukuzwa.”

Mtoa taarifa hizi ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya Rais Kikwete.

Kuvuja kwa taarifa kwamba Lowassa, Rostam na Chenge wameapa “kufa na Kikwete” iwapo ataendelea na kinachoitwa msimamo wake wa kutaka kuwaondoa ndani ya uongozi wa juu wa CCM, kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa watuhumiwa hao wa ufisadi walikutana kwa faragha na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Msekwa na kugoma kujiuzulu.

Katika mkutano huo, Rostam alisisitiza kuwa hawezi kujiuzulu kwa kuwa hana hatia. Hakukuwa na habari yoyote kuhusiana na mazungumzo kati ya Chenge na Msekwa.

Bali Lowassa alihoji sababu ya kutakiwa kujiuzulu na baada ya kuelezwa kuwa ni tuhuma za mkataba tata wa Richmond, haraka alijibu, “Kuhusu Richmond, ukweli unafahamika… Rais anafahamu hilo na kila mmoja anajua hilo.”
Mtoa taarifa anasema Lowassa katika kuhakikisha anabaki ndani ya chama hicho amepanga kueleza mkutano wa NEC, hatua kwa hatua, jinsi kampuni ya Richmond na Dowans zilivyoingia nchini na jinsi zilivyopewa mkataba.

Inadaiwa kuwa hatua hiyo ya Lowassa inatokana na Kikwete kuvunja kinachoitwa “makubaliano ya awali” ya kumsafisha kuhusiana na sakata hilo.

“Unajua Kikwete na Lowassa walikuwa na makubaliano, kwamba yeye ajiuzulu (uwaziri mkuu Februari 2008) ili kulinda serikali na chama. Kisha wakakubaliana kuwa Kikwete atafanya kazi ya kumsafisha kupitia chama na Bunge.

“Lakini Kikwete hakutekeleza makubaliano hayo kwa kisingizio kuwa ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa. Sasa yeye ameamua kujisafisha mwenyewe,” taarifa zinaeleza.

Bali si siri kwamba Rais Kikwete, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, alifika Monduli, katika jimbo la Lowassa, kumshika mkono, kuuinua na kumtangaza mkutanoni kuwa ni kiongozi shupavu anayestahili kupigiwa kura.

Lowassa anasemekana kutoridhishwa na kauli hiyo katika harakati zake za kurejea ulingo wa juu wa siasa nchini.

Katika mkutano kati ya Lowassa na Msekwa, habari zilinukuu viongozi hao, kila mmoja akishupalia mwenzake.

Wakati imeripotiwa Msekwa akisema, “Lowassa acha mbio za urais,” Lowassa yeye alijibu mapigo kwa kusema, “Lini nimetangaza kugombea urais? Je, (kama nilitangaza) haramu kufanya hivyo, au kuna mliowaandaa?”

Imeelezwa kuwa Msekwa alikana kuwapo mtu aliyeandaliwa, lakini akasema, “ndivyo wanavyosema, kwamba wewe unataka urais,” na kwamba “…haya mambo ya urais yatatuvuruga.”

Wakati Lowassa akipanga kujisafisha kwenye NEC, taarifa zinasema Rais Kikwete amepanga kuitumia Kamati Kuu (CC), “kuwafukuza watuhumiwa” ili kujenga sura ya uwajibikaji.

Ni ndani ya kikao hicho maalum cha CC, ambamo inadaiwa Rais Kikwete amepanga kupeleka hoja ya kuwafukuza watuhumiwa hao, halafu kuijulisha NEC kwa njia ya taarifa.

Inadaiwa mara hoja hiyo itakapoingia NEC, Kikwete atawaeleza wajumbe kuwa CC imetekeleza maagizo ya NEC iliyopita ambayo inadaiwa iliagiza kufukuzwa chama watuhumiwa wote wa ufisadi.

Hata hivyo, kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ndani ya CCM amesema, iwapo Kikwete ataamua kutumia njia hiyo, basi ajiandae kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa kundi la Lowassa na wafuasi wake; jambo ambalo linaweza kusababisha kugeuziwa kibao na kuishia kujadiliwa utendaji wake ndani ya chama na serikali.

“Hapo ndipo hata ile hoja ya kutenganisha kofia mbili inaweza kuibuka. Unajua ndani ya CCM kuna viongozi wengi wanaomuona Kikwete ni dhaifu na hivyo wanataka kutenganisha kofia ya mwenyekiti wa chama na rais wa nchi. Sasa akifanya mchezo hapa kunaweza kutokea makubwa,” ameeleza mmoja wa viongozi wa CCM ambaye ni mwanasheria.

Anasema, “Kamati Kuu ya chama haina uwezo wa kuwafukuza wale jamaa. Ni lazima kama wanataka kuwafukuza, hoja iletwe NEC, kwani hiyo ndiyo inayofanya kazi kwa idhini ya mkutano mkuu. Sasa mle NEC, hawa jamaa wako vizuri. Kikwete akileta hoja hiyo, anaweza kujikuta anaingia katika mgogoro na pengine chama kugawanyika.”

Nguvu ya Lowassa inatarajiwa kuegemea viongozi wastaafu, hasa Rais Benjamin Mkapa ambaye wachambuzi wa mambo wanamchukulia kuwa hawezi kukubaliana na mpango wa Rais Kikwete wa kufukuza wenzake katika chama.

Mkapa ambaye amejitosa katika kesi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, anachukuliwa na wengi kuwa hafurahishwi na hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama na hata serikali chini ya Rais Kikwete.

Kwa mujibu wa watu waliokaribu na viongozi wa juu CCM, hoja ya kumfukuza Lowassa na wenzake tayari imeiva na kwamba azimio la kuwafukuza litafikishwa CC “kwa ajili ya kubarikiwa tu.”

0
Your rating: None Average: 4 (8 votes)
Soma zaidi kuhusu:
Waandamanaji ambao wanasema wazi kuwa wanapigania uhuru, heshima, haki na usawa. cheap advertising|made in china

Mimi kupakuliwa makala juu ya suala wiki kadhaa iliyopita kutoka picktorrent search http://www.picktorrent.com na kuwa na uhakika yangu mwenyewe ya maoni juu ya mambo yote. Mtanzania naungana na wewe japo kiingereza chako hakijanyooka inavyo takiwa lakini kile ulicho lenga nimekielewa, ni kweli huyu jamaa haja tulia, anafanya mambo kinyemela , na speech amabayo anayo toa haiendani na ukweli sijui kwa sababu hawajui kinachoendelea huku lakini I hope so kuna watu ama watanzania ambao wanaishi huko wanao jua inshu nzima , lakini cha msingi anajaribu kujiaibisha yeye mwenyewe,inatakiwa kila apo enda atangaze biashara halali na wala sio kutangaza uongo.

lets change the way we think towards our president,let us be positive withiout hesitate to speak the truth, Kikwete is responsible for all what is happening in Tanzania,he is the major source,anajua kila kitu alichofanya lowasa na lowasa ana siri kubwa ambayo ipo siku ataitoa tu atakubali afe peke yake atakuja kufungua mdomo wake tu we ngoja kwamba Mr president knows everything about all the ufisadi issues, time will tell
Lowasa hana nguvu kama watu wanavyompamba. Kinachomsaidia ni udhaifu wa Kikwete. Kikwete salama yake na chama chake ni kuwatimua hawa wezi ingawa sina hakika kama naye si mwizi.
Si kwamba Lowasa hana nguvu kama watu wanavyomthania, bali Lowasa anaweza kuwa na nguvu kutoka na support ya watu hasa anakotokea. Pia hatuwezi kumuita Lowasa ni mwizi wakati ushahidi hatuna,chombo pekee kinachoweza kuprove kwamba Lowasa ni mwizi au si mwizi ni Mahakama pekee kam chombo cha kutafsiri sheria.
Mheshimiwa mbunge Rostam anapokea maoni na ushauri wenu hapa http://www.tathmini.com/Pages/Details/1/azizi-abdulrasul-rostam kuhusu utendaji wake. Kazi kwenu
Toa maoni na kura zako kuhusu utekelezaji wa Wabunge na mawaziri Tanzania hapa http://www.tathmini.com/pages
Hivi kweli nani anao ushahidi wa kutosha kwamba Lowasa ni fisadi?Lowasa alitolewa kafara kwa sababu ambazo ni za kisiasa tu na ni vema jutenge utamaduni wa kujiaminisha kwa jambo kabla ya kuwasulubisha watu. Lowasa mwenyewe anajua vizuri sababu za yeye kutoswa na ndio maana wakati anajiuzulu alisema najua kinachotafutwa ni uwaziri mkuu. Namhurumia sana Lowasa, katendewa mambo mengi mabaya na kunyamaza, sasa ameamua kuamka usingizini na kusema..ameikatalia hata CCM yenyewe na CCM wamenyamaza. Tusimuue Lowasa yule mchapa kazi. Hata mimi nilimlaumu sana Lowasa lakini sasa nimeamua kutafakari upya juu ya ufisadi wa Lowasa..ila Lowasa naye atuambie kilichifichwa chini ya Dowans..hilo tu lakini ukweli umeanza kujulikana juu ya Lowasa, CCM na Kikwete mwenyewe.
Katika harakati za kukimegea hekima chama chake alichokiasisi Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya, tena muda mfupi kabla hajatutoka kwamba hakuna Rais atakayeingia madarakani kwa njia ya rushwa anayeweza kupambana kikamilifu na rushwa. Haya sasa yamedhihirika baada ya Kikwete kupigiwa kampeni kwa fedha chafu za mafisadi na EPA na hatimaye kupenyezwa madarakani na mafisadi papa ambao vivuli vyao vinamfanya aweweseke hadi leo hii. Inashangaza sana kuona walewale aliokuwa akiwaamini kama watetezi wa kile alichokiamini ndiyo walikuwa wa kwanza kuyafungua makucha yao na kufanya kufuru ya ufisadi wa kutisha mara tu baada ya kifo chake. Ilikuwa kana kwamba walikuwa wakimwombea afe ndiyo wafanye hujuma hiyo. Ni kuanzia baada ya kifo cha mwanamapinduzi huyu CCM ilipoteza kabisa uelekeo na kujitoa kwa wakulima na wafanyakazi na badala yake kuwa chama cha wezi, vibaka, mafisadi na wahujumu uchumi. Ni katika wakati huhu huo mali na amali za taifa zilihujumiwa vya kutisha, kuanzia ardhi hadi nyumba watu waligawana! Sote tu mashahidi wa jinsi CCM ilivyokuwa ikiitisha "Harambee" za kutafuta michango toka kwa wafanyabiashara wengi wao wakiwa wezi, vibakauchumi na mafisadi papa. Haya ndiyo matokeo ya serikali inayomilikiwa na mafisadi waliojipenyeza mpaka kwenye "Injini" ya dira ndiyo chama. Kwa sasa ni vigumu kumpata aliye safi ndani ya CCM, na kama yupo basi hana mahusiano mema na wenzie. CCM imekwenda kinyume cha kila aina ya mafundisho waliyoaswa na mwasisi wao. Aliwaonya juu ya udini na ukabila akisema "kiongozi makini huzungumzia sera za nini atafanya kwa ajili ya nchi yake, lakini kiongozi aliyefilisika atazungumzia udini na ukabila" Je kuna hata chembe ya mashaka kwamba CCM wametenda kinyume cha nasaha hizo? Sisi sote tu mashahidi jinsi walivymdhalilisha kada wao kwa kumwita mwarabu na kumhusisha na mauaji ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar! Na leo hii tunashuhudia Rais mzima akipanda jukwaani kuimba wimbo wa udini huku mwangi wake upipaazwa na viongozi wasio makini wa kidini wenye kujipendekeza kwa manufaa binafsi! Laana ya Baba wa Taifa hili inaitafuna CCM na sasa wamelewa na kuviimbiwa sumu ya ufisadi waliyoichangamkia fasta fasta tangu kifo cha muasisi wao aliyeonekana kuwaletea giza na bughudha dhidi ya harakati zao chafu ambazo sasa ndiyo wanahunyahunya kuondokana nazo. CCM wana chaguo mbili tu, nazo ni kufanya usanii sanii na kuachana na sera zao za kujivua magamba ambazo kwa kweli hazitekelezeki kwani karibu wooote wameshaonja ladha ya ufisadi, au wachukue hatua za papara za kuwang'oa maswahiba wao na kuangukia pua mara moja! Waziri Mkuu Pinda alishawahi kusema kwamba mafisadi wana nguvu za kutisha na kupambana nao bila ya tahadhari kunaweza kuiyumbisha serikali. Je sasa wakati umefika wa serikali iliyowekwa na hawa hawa watu kupambana nao na kuikabidhi mikononi mwa umma? Tusubiri, tuone. Muda utaamua. Mungu ibariki Tanzania.

Heri yao masikini walio huru kuliko matajiri waishio katika utumwa

ni habari njema kwetu..
fidiboy
KIKWETW HASIMWOGOPE MTU KAMA KWELI ANA NIA NZURI NA CHAMA.
SIXBERT
Hii ni habari njema sana, naona sasa tunakaribia mwisho wa CCM. Tuombe tu huu mvurugano uendelee wagawanyike watoke madarakani, nchi ianze kupiga hatua za maendeleo sasa!!
Babu