Mafuriko ya kihistoria yaivuruga Pakistan


Mwandishi wetu's picture

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 01 September 2010

Printer-friendly versionSend to friend

AFYA

Wizara ya Afya tayari imetoa taarifa kwamba mafuriko yameharibu asilimia tano ya huduma na hiyo inatajwa kama ni changamoto kubwa hata kufikia huduma kurudia kawaida.

Watoto karibu milioni 3.1 wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wako hatarini kuambukizwa magonjwa yanayotokana na ulaji na unywaji wa maji machafu.

Tayari Shirika la Afya Duniani (WHO) limebashiri kuwepo ongezeko kubwa la watu watakaopata magonjwa kama kipindupindu na matumbo ya kuharisha katika kipindi cha wiki nne hadi sita zijazo.

Maeneo mengi yamekuwa vigumu kufikika ili kuwapatia huduma za dharura watu walioathiriwa na mafuriko hayo.

USALAMA

Mashirika mengi ya misaada ya Umoja wa Mataifa yanahudumiwa na watumishi wanaotoka nchi za magharibi. Tatizo ni kwamba kuna ugumu kwao kuhudumia Sindh.

Hiyo inatokana na mji huo kupakana na maeneo ya Afghanistan, jirani wa Pakistan ambako wapiganaji wa Taliban wanashikilia maeneo hayo na wangefurahi kukutana na wafanyakazi hao.

Majeshi ya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Ulaya Magharibi (NATO) ndiyo yanayopambana na Taliban huko na matokeo yake wapiganaji hao wanaona raia wote wa Ulaya na Marekani adui zao wakuu.

Shida zinazowakabili raia walioathiriwa na mafuriko zinaweza kuwa chanzo kikubwa cha matatizo ya usalama; hususan iwapo hawatapata mapema huduma za dharura.

Tayari kuna taarifa za matukio ya fujo katika maeneo ambako kuna upungufu mkubwa wa dawa, maji safi, mablanketi na mashuka.

Tatizo ni kwamba walinzi wa usalama ni wachache katika maeneo hayo kuliko wale wanaotakiwa. Na wengine hawawezi kuwasili haraka iwezekanavyo kwa vile njia kuu za usafiri kwenda maeneo walipo wenye shida hazipitiki.

0
No votes yet