Majina makubwa yaongoza kufelisha


Joster Mwangulumbi's picture

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 15 February 2012

Printer-friendly version

MWAKA jana serikali ilisifu shule za sekondari za kata kwamba zina ubora unaohitajika baada ya wanafunzi saba kati ya 10 walioongoza kitaifa mtihani wa kidato cha VI kuwa miongoni mwa waliosoma shule hizo.

Serikali haikutaka kujishughulisha na maelfu ya waliofeli kutoka shule hizo za kata. Halikadhalika mwaka huu, serikali inafurahia wachache waliofanya vizuri kutoka shule hizo.

Ukweli shule hizo zimekuwa kama kijiwe cha kushindia watoto; wanafunzi wengi wanatoka na sifuri, na mfano mzuri ni matokeo ya shule zilizopewa majina ya watu maarufu au viongozi wa nchi.

Matokeo ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2011 kutoka shule hizo ni mabaya. Sampuli ya matokeo ya shule zenye majina ya marais, waliopata kuwa mawaziri wakuu na makatibu wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanaonyesha wengi wamefeli.

Shule ya Sekondari ya Yusuf Makamba ya jijini Dar es Salaam ndiyo inaongoza kwa kufelisha wanafunzi.

Kwa mujibu wa matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2011 yaliyotangazwa wiki iliyopita na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, zaidi ya nusu ya wanafunzi wote wamefeli.

Matokeo yanaonyesha DI = 1, DII = 7, DIII = 18, DIV = 139, na waliofeli ni = 185. Matokeo ya mwaka 2011 ni bora kiasi kuliko 2010 kwani yalikuwa DI=2, DII=4, DIII=19, DIV=113 na waliofeli 314.

Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa ya jijini Dar es Salaam ambayo ilipewa jina kwa heshima ya Rais wa Awamu ya Tatu, pamoja na kujitutumua katika daraja la kwanza bado imefilisha wengi.

Matokeo kamili yanaonyesha DI = 19, DII = 39, DIII = 69, DIV = 189, na sifuri 137. Mwaka 2010 matokeo yalikuwa DI=5, DII=25, DIII=74, DIV 263 na sifuri 282.

Mwinyi sekondari ya Pwani iliyopewa jina kwa heshima ya Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hasaan Mwinyi imefelisha 111. DI = 0, DII = 0, DIII = 0, DIV = 35 na sifuri 111.

Lakini matokeo ya Shule ya Kiislamu ya Ali Hassan Mwinyi ya Tabora yanaonyesha DI = 0, DII = 0, DIII = 4, DIV = 60 na sifuri 56. Shule hiyo mwaka 2010 ilifaulisha kiwango cha DI=0, DII=3, DIII=2, DIV=38 na waliofeli 67 wakati Barabara ya Mwinyi ina DI = 2, DII = 2, DIII = 12, DIV = 78 na sifuri 87.

Mikoa au wilaya nyingi zimejitokeza kutumia jina la hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika shule nyingi. Matokeo ya shule hizo hayaendani kabisa na heshima ya jina hilo.

Shule ya Sekondari ya J.K.Nyerere ya Kilimanjaro ina DI = 4, DII = 15, DIII = 23, DIV = 103 na sifuri 71; Mwalimu Nyerere Sekondari ya Shinyanga imefaulisha kiwango cha DI = 2, DII = 3, DIII = 18, DIV = 112 na sifuri 34.

Katika Shule ya Nyerere Memorial ya Tanga DI = 2, DII = 2, DIII = 18, DIV = 74 na sifuri 74; Mwalimu J.K.Nyerere ya Mbeya ina DI = 0, DII = 2, DIII = 12, DIV = 42 na sifuri 54, na mwaka juzi ilipata DI=0, DII=4, DIII=10, DIV=42 na waliofeli 43 wakati Nyerere ya Unguja ina DI = 0, DII = 0, DIII = 12, DIV = 227 na sifuri 29.

Matokeo katika Shule ya Kambarage ya Mara ina DI = 0, DII = 0, DIII = 1, DIV = 36, na sifuri 91.  Mwaka juzi ilipata DI=1, DII=3, DIII=10, DIV=90 na waliofeli 105.

Shule nyingine zilizojitahidi kufelisha badala ya kufaulisha ni zilizopewa jina la Rais Jakaya Kikwete. Shule ya J.M.Kikwete ya Mbeya imepata DI = 1, DII = 3, DIII = 5, DIV = 38 na sifuri 60. Mwaka 2010 ilipata DI=0, DII=4, DIII=2, DIV=29 na waliofeli ni 52.

Jakaya Kikwete Sekondari ya Manyara imepata DI = 0, DII = 1, DIII = 4, DIV = 54 na sifuri 39; Jakaya ya Mbeya DI = 0, DII = 0, DIII = 1, DIV = 14, na sifuri 24 huku iliyopewa jina la mkewe, Salma Kikwete ya Dar es Salaam imepataDI = 1, DII = 4, DIII = 10, DIV = 125, na sifuri 132.

Matokeo ya shule zenye jina la Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein hayasadifu umahiri wa kiongozi huyo. Shule ya Dr. Ali M. Shein ya Singida ina DI = 0, DII = 0 DIII = 1, DIV = 17 na sifuri 20; na Dr. A.M.Shein ya Ruvuma ina DI = 0, DII = 0, DIII = 0, DIV = 14 na sifuri 26. Mwanamwema Shein ya Singida imepata DI = 0, DII = 1, DIII = 1, DIV = 18 na sifuri 36.

Matokeo ya shule nyingine zenye majina ya watu ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu au makatibu wakuu ni Lowassa ya Arusha DI = 0, DII = 2, DIII = 11, DIV = 95 na sifuri  44; huku Regina Mumba Lowassa ya Dodoma ikitoka na DI = 0, DII = 0, DIII = 1, DIV = 11 na ziro 23.

Pius Msekwa ya Mwanza DI = 1, DII = 3, DIII = 8, DIV = 64 na sifuri 73; Sumaye Buziku ya Kagera DI = 0, DII = 0, DIII = 5, DIV = 42 na sifuri 20.

Sumaye ya Manyara DI = 0, DII = 0, DIII = 1, DIV = 22 na sifuri 50 na matokeo ya F.T Sumaye ya Manyara ina  DI = 0, DII = 1, DIII = 5, DIV = 47 na sifuri 60.

Philip Mangula ya Iringa DI = 0, DII = 8, DIII = 17, DIV = 136 na sifuri 26; Aboud Jumbe ya Dar es Salaam DI = 2, DII = 7, DIII = 20, DIV = 83 na ziro 99; Rashid Mfaume Kawawa ya Lindi DI = 0, DII = 1, DIII = 2, DIV = 36 na sifuri 118.

Baadhi ya viongozi hawakuomba wala kushawishi ili shule zipewe majina hayo kwa heshima ya utumishi wao. Lakini kwa vigezo vyovyote viwavyo matokeo haya yanaaibisha majina hayo, hivyo viongozi wa shule husika na wale wa serikali, wanatakiwa kusimamia vizuri utoaji wa elimu ili kuhakikisha majina hayo yanabaki na hadhi inayolingana na utumishi wao.

0
No votes yet