Rais Kikwete aumbuka


Saed Kubenea's picture

Na Saed Kubenea - Imechapwa 14 April 2010

Printer-friendly versionSend to friend
Rais Jakaya Kikwete

KUMBE Rais Jakaya Kikwete hakusoma sheria aliyosaini kwa mbwembe. Sasa baada ya kugundua kasoro zake anataka ikarabatiwe kwa njia ya kanuni, MwanaHALISI limeelezwa.

Hilo liligundulika katika mkutano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wenyeviti na makatibu wa wilaya uliomalizika wiki iliyopita mjini Dar es Salaam.

Taarifa za ndani zinasema, bila aibu na hasa kwa ujasiri wa kiongozi mkuu wa nchi, Rais Kikwete alimuuliza Philip Marmo, waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, maana ya baadhi ya vifungu katika sheria hiyo.

Lakini katika hali ambayo haikutegemewa, Marmo alijibu kana kwamba anamkejeli rais, jambo ambalo lilistua wajumbe wa kikao hicho cha juu cha utekelezaji wa sera za chama.

MwanaHALISI limeelezwa kwamba Rais Kikwete alistushwa na kifungu cha sheria kinachotaka mgombea kuwasilisha katika ofisi za msajili, taarifa ya fedha atakazotumia.

Kifungu hicho kinatoa siku saba kabla ya siku ya mwisho ya NEC kutangaza majina ya wagombea.

Kifungu kingine kinachodaiwa kumstua kinahusu idadi ya wajumbe wa kampeni. Kwa CCM, yenye hata vikundi vya ngoma na nyimbo kama ToT, kuweka timu ndogo kunaweza kupunguza shamrashamra na kuathiri kampeni.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, ilikuwa baada ya rais kupitia maeneo hayo, alimuuliza Waziri Marmo iwapo kile alichokuwa akifafanua kimetokana na sheria iliyopitishwa.

Naye Marmo, akiongea kwa sauti ya unyenyekevu alijibu, “…hiki ndicho ulichosaini.”

Kwa kauli ya Marmo, Rais Kikwete alionekana kustuka na kusema, kama hali ni hivyo, basi sheria itakuwa imeingilia hata mchakato wa wagombea ndani ya vyama, kimeeleza chanzo chetu.

Taarifa zinamnukuu rais akihoji kwa nini “sheria imekwenda mbali mno” na kuagiza papohapo kuwa wahusika waangalie ambapo sheria inaingiliana na watengeneze kanuni zitakazoleta nafuu.

Rais amenukuliwa akimwagiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutengeneza “kanuni vizuri” ili kuondoa mwingiliano unaoleta ugumu wa utekelezaji.

Hoja ya maelekezo ya sheria mpya ya gharama za uchaguzi ilikuwa moja ya ajenda za kikao cha NEC, wenyeviti na makatibu wa CCM wilaya kutoka kote nchini.

Tarehe 17 Machi mwaka huu, Rais Kikwete alisaini hadharani na kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ikulu Dar es Salaam ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na majaji, wabunge, viongozi wa serikali na vyama vya siasa, mabalozi na waandishi wa habari.

Hata hivyo, sheria hii imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya siasa na wanaharakati, kabla na baada ya kusainiwa kuwa itakuwa ya udhibiti kwa wenye msimamo tofauti na watawala.

Aidha, siku tatu baada ya sheria hiyo kusainiwa, mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa alitupa kombora kwa kusema sheria aliyosaini rais ilikuwa na vipengele ambavyo havikujadiliwa bungeni na kwamba “viliingizwa kinyemela.”

Ubishi wa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Jaji Frederick Werema kwamba hakukuwa na chochote kilichofanywa kinyemela ndio umekuza hoja ya Dk. Slaa na kufanya achimbue zaidi kshfa hiyo.

Katika kufukua, Dk. Slaa amekwenda hadi kwenye kumbukumbu za bunge (Hansard) na kuthibititisha kuwa Kifungu 7 (3) ambacho kimo katika sheria aliyosaini rais hakikujadiliwa bungeni na hivyo hakikurekodiwa katika hansard.

Mtunga sheria huyo kutoka Karatu amesema pia kuwa chochote kilichojadiliwa bila kuamuliwa na bunge kilikuwa kinatarajiwa tu katika kanuni au fafanuzi za au ainisho za maneno na taratibu lakini siyo katika vifungu vya sheria.

Katika majibu yake kwa kauli za Dk. Slaa, Jaji Werema alitetea serikali na kuthibitisha kuwa kifungu hicho kiliwekwa na waziri Marmo.

Dk. Slaa amesema katika andishi maalum, “Hakuna mwenye mamlaka, hata rais hana mamlaka hayo, sembuse waziri.

“Baada ya mjadala katika Kamti ya Bunge zima, maneno yakikubaliwa ndiyo hayo yanaingia kwenye sheria na serikali haina mamlaka ya kwenda kuyarekebisha inavyotaka. Ndiyo maana ya kusema ‘kifungu kimepitishwa,’ ” ameeleza Dk. Slaa.

Akiweka msisitizo, Dk. Slaa anasema, “Kitendo cha kuchomeka kinyemela ni kitendo kibaya sana na kinapaswa kulaaniwa, kwa sababu, kwa utaratibu huu wataalam wanaweza kuipeleka nchi pabaya kwa kupenyeza jambo lolote wanalotaka wao hata kama halijajadiliwa au limekataliwa na Bunge.”

Dk. Slaa anafafanua hatua ya serikali ya kuingiza mambo kinmyemela katika sheria kuwa ni kosa la jinai na kusema hata kifingu walichochomeka kinyemela kina madhara makubwa.

Kifungu kilichoongezwa na serikali kinataka timu ya kampeni kukaguliwa na watendaji wa serikali ya CCM.

“Kampeni ndiyo inayobeba mikakati na siri yote ya uchaguzi. Haiingii akilini kabisa kuwa serikali (pengine unayotaka kuiondoa kwenye uchaguzi ambayo ndio haki ya msingi ya kila mgombea) ndiyo inaweka mkono wake kwenye udhibiti wa mikakti hiyo,” anafafanua Dk. Slaa.

Anasema kuweka kifungu kama hicho ni “wenda wazimu, kwa mtu yeyote aliyefikiria jambo hilo, au anaandika tu kutoka mezani na au hajui maana halisi na majukumu yake.”

Kutokana na kuibuka kwa kashfa hii, serikali sasa imeamua sheria hiyo irejeshwe bungeni ili kufanyiwa marekebisho yanayostahili.

Naye Dk. Slaa tayari ametoa pendekezo: “Namna pekee ya kuepukana na athari hiyo ni kwa serikali kukiri imefanya makosa, na ndio ustaarabu bila kutafuta visingizio.”

Anasema serikali iwasilishe kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge hili ulioanza jana, kitu kinachoitwa “Miscellaneous Amendment” – marekebisho ya sheria mbalimbali – na au ikichelewa sana katika Bunge la Bajeti.

Wachunguzi wa mambo wanasema Rais Kikwete atakuwa amesikitishwa sana na hatua ya wasaidizi wake ya “kumchomekea” vitu ambavyo baadaye vinamomonyoa hadhi yake kama mkuu wa nchi.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa wamempotosha au wameshindwa kumsaidia rais, ni pamoja na Jaji Werema ambaye ametetea uingizaji kinyemela kipengele ambacho hakikujadiliwa bungeni.

Mwingine anayetajwa ni waziri Marmo ambaye ambaye nduye hasa ametajwa kubuni na kuingiza maneno ya kifungu kinacholaaniwa.

0
Your rating: None Average: 3 (3 votes)
Soma zaidi kuhusu:
Hata wakati wa kurithi mkataba wa uzalishaji umeme kutoka iliyoitwa kampuni ya Richmond, hakunyanyua mguu kutoka Oman. free advertising|Hospital beds

hakutumia aakili ndio maaan anaendesha nchi kip[mbavu

nadhani kila aliyeweka maoni yake amekuwa na jambo moja kubwa nalo ni kuweka matoleo ya gazeti la wiki mapema. naelewa pia kwa upande wa kibiashara mnakuwa na wasi wasi lakini ukweil unabaki kuwa njia za kuuza matangazo zipo na kama mnavyoelewa kuwa gazeti lenu lina wasomaji makini kwahiyo mnaweza kabisa kuwashawishi makampuni mbali mbali yakatangaza kwenye tovuti yenu na nyie mkapata pesa ziada lakini pia kumbuka kuwa wenye nia njema na wenye kuwa na umakini hawapo Tanzania peke yake lakini ni watanzania tena naweza kusema Watanganyika wa ndani kabisa wenye uchungu na nchi yao tafadhalini msiwanyime fursa ya kuona matukio kwa wakati na kusoma habari kwa wakati hivyo jitahidini kuweka matoleo kwa wakati na inawezekana kikubwa ni nia tu
Ahsante

Inawezekanaje Rais akasign such an important piece of legislation bila kusoma. Is it possible to absolve him of the blame given the amount of resources at his disposal?!! I think it is a case of complete negligence and incompetence. Raisi hayupo hapo kuletewa tu documents and sign. I dont think we elected a rubber stamp president who has no time to review the papers before him and sign without proper application of mind. If he has been doing so its high time we advise him to change.

Matatizo ya kudanganywa na wasaidizi hayajaanza jana. There is enough evidence for that. What is troubling is after knowing that he still puts 100% in the same people and the through the same procedure!!

It is embarrasing that the president becomes aware of the faulty provisions of a law in his party meeting and orders the re-examination of the same!. A serious question then needs to be asked on whether the proposed changes will not only benefit his party? Besides in his capacity in that meeting as the party chairman,did he even have the authority to order that? (Because that was a party meeting so he was not discharging his executive functions)

Mimi ombi langu ni kama huyo msoamaji wa kwanza, ya kwamba muwe mnaweka matoleo mapema kwenye mtandao. pili kuhusu hilo la rais, mara nyingi rais amekuwa akidanganywa mambo mengi kama lile la arusha, la kugawa gari la wagonjwa nk. huenda mambo mengi zaidi anapotoshwa na kuweza kuirudisha nchi yetu nyuma.

uniseni

Safi sana mwanahalisi. Gazeti lenu sasa linapendeza kwenye mtandao. Naomba muwe mnawehi kuweka matoleo mapema.