Rostam ndiye Dowans

MJUMBE wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ni moja ya nguzo kuu ndani ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans, imefahamika.
Kwa maana hiyo, Rostam atakuwa mmoja wa watakaofaidika na mabilioni ya shilingi pale serikali itakapokubali kulipa Dowans Sh. 94 bilioni kwa kile kinachoitwa fidia za kuvunja mkataba.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa, hata kabla ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) kuwepo – kwani usajili wake una utata mkubwa – tayari Rostam alikuwa “amepewa” nguvu ya kisheria (Powers of Attorney) ya kusimamia shughuli za kampuni hiyo.
Nyaraka za Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), zinaonyesha kuwa Rostam alipewa mamlaka hiyo 28 Novemba 2005.
Bali kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) inadaiwa kusajiliwa Februari 2007, miaka miwili baada ya Rostam kupewa mamlaka ya kisheria ya kuiwakilisha.
Haikufahamika Rostam alikuwaje na mamlaka hiyo kabla kampuni haijaundwa; na bado uundaji na usajili wake haujathibitika kuwa halali.
Ofisi ya msajili wa makampuni nchini Costa Rica, alimwandikia Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, 3 Agosti 2008 akieleza kuwa Dowans Holdings SA haimo kwenye orodha ya makampuni ya nchi hiyo. Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez.
Aidha, taarifa zinasema wakati Rostam anakabidhiwa nguvu hiyo ya kisheria, mkataba kati ya Shirika la umeme la Taifa (TANESCO) na kampuni ya kufua umeme ya Richmond Development Company (LLC), ulikuwa haujasainiwa.
Mkataba kati ya TANESCO na Richmond ulisainiwa 23 Juni 2006, mwaka mmoja kabla tarehe inayodaiwa Dowans ilisajiliwa na karibu miaka miwili kabla Richmond “kubadilishana” mkataba na Dowans.
Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans tayari wamewasilisha Hazina, ankara ya madai yake ikitaka serikali kuilipa kinyume cha taratibu.
Tarehe 17 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yeyote ya hisa kwenye makampuni matatu – Dowans Tanzania Limited, Dowans Holding SA na Richmond. Alikana pia kufahamu wamiliki wa makampuni hayo.
Bali kutajwa kwake katika shauri hilo kuwa ndiye msimamizi wa Dowans Holdings SA (Costa Rica), kunaweza kuchukuliwa kuwa, ama amekuwa akificha ukweli au akisema uwongo kuhusiana na suala hilo.
Rostam ndiye amekuwa akitajwa pia katika ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu ya Taifa (BoT) kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited. Mara zote amekana.
Kwa mujibu wa nyaraka za ICC, Mwenyekiti wa mahakama hiyo, Gerald Aksen na wasuluhishi wenzake wawili, Jonathan Parker na Swithin Munyantwali, walijiridhisha na kiapo kilichompa Rostam mamlaka ya kusimamia maslahi ya Dowans.
Katika hukumu yake, ICC inasema TANESCO inaamini kuwa Dowans Holdings SA (Costa Rica), ni “taasisi ya, au inasimamiwa na, au ni kitu kinachomhusu Rostam Aziz, mwanasiasa wa Tanzania.”
Kwenye ukurasa wa 121 wa hukumu hiyo, ICC inasema jitihada za TANESCO kupinga uhalali wa Dowans kulipwa mabilioni hayo ya shilingi, zilikosa nguvu kwa kuwa shirika hilo halikukataa kusaini mkataba na Dowans hata hata pale lilipotambua utata wa Richmond.
Wakati hayo yakiibuka, taarifa zinasema Richmond, ambayo haikuwa halali kisheria, haikuwa na uwezo kifedha wala kitaaluma, inasubiri Dowans walipwe ili nayo “ichukue chake.”
Kuna taarifa kuwa wanaoitwa wawakilishi wa Richmond, wanadai kuwa walizalisha umeme wa megawati 20 kabla hawajafungishwa virago.
Wachunguzi wa mambo wanasema kile ambacho Richmond wanasubiri, ni hichohicho ambacho wanasubiri wote waliosaidia kuipa kampuni hiyo mkataba kwa upendeleo.
Taarifa zinasema wawakilishi wa “Richmond hewa” wanataka kuiomba mahakama kuzuia malipo kwa Dowans hadi hapo mahakama itakapolipatia ufumbuzi shauri lao.
Alhamisi iliyopita, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitaja, mbele ya waandishi wa habari, wakurugenzi wa Dowans, huku akishindwa kueleza lolote kuhusu uhusiano wa Rostam na Dowans.
Kushindwa kwa Ngeleja kumtaja Rostam kunatokana na madai kuwa kabla ya kuwa mbunge na waziri, Ngeleja alikuwa mtumishi wa kampuni ya Vodacom ambako Rostam alikuwa mmoja wa wakurugenzi.
Katika hali inayothibitisha umiliki wa kampuni hiyo kugubikwa na utata, Ngeleja alitaja kampuni ya Portek International ya Indonesia kuwa ni miongoni mwa wana hisa ndani ya Dowans Holdings SA (Costa Rica). Alisema inamiliki asilimia 39 ya hisa za kampuni hiyo.
Lakini MwanaHALISI limegundua kampuni ya Portek International haina uhusiano na Dowans Holdings SA.
Bali Portek International iliyotajwa na Ngeleja, ni moja ya makampuni tanzu ya Portek Systems and Instruments ya Singapore chini ya shirika lake la Portek Engineering Holdings Pte, inayomiliki asilimia mia moja ya hisa za Portek International.
Hadi mwaka 2008 kampuni hiyo ya Indonesia haikuwa na hisa yoyote katika Dowans Holdings SA wala haikuonesha kuwa wanaitambua kwa namna yoyote ile.
Portek International ni kampuni inayohusiana na huduma za bandari sehemu mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa tovuti yake ya http://www.portek.com.
Shughuli nyingine zinazofanywa na Portek International iliyoanzishwa mwaka 1988, ni pamoja na kuboresha vifaa na mashine zinazotumika bandarini, kubeba makontena, kukodisha vifaa hivyo kwa makampuni mengine duniani, kuuza vipuri vya mashine na kutoa ushauri wa kitaalam katika kuendesha huduma za bandari.
Kwa muda wa miaka yote hii mitano tangu sakata la Dowans lianze, kampuni ya Portek haijawahi kutajwa au yenyewe kuitaja Dowans Tanzania Limited au Dowans Holdings SA kuwa ni miongoni mwa makampuni yake tanzu.
Zaidi ya yote, katika ripoti za kila mwaka kuanzia 2006, kampuni hiyo haijaonyesha mahali popote kumiliki kampuni ya Dowans Tanzania Limited.
Taarifa zinasema kama kweli Dowans Tanzania Limited, ingekuwa inamilikiwa na kampuni hiyo, basi ni lazima wangeitaja, hasa kutokana na kubanwa na sheria za uuzaji hisa katika soko la hisa la New York, nchini Marekani.
Katika soko la hisa la New York, kampuni ya Portek International inatumia alama ya PORT:SI.
Kutokuonekana kwa kampuni ya Dowans kuwa sehemu ya orodha ya makampuni ya Portek International, kunaacha maswali mengi kwa kauli ya waziri Ngeleja aliyeitaja.
Hata hivyo, imefahamika kuwa kamapuni ya Portek International ina uhusiano wa kibiashara na kampuni ya TICTS ambayo mmoja wa wakurugenzi wake ni Nazir Karamagi.
Kampuni hiyo ndiyo iliyoingiza nchini winchi zinazotumiwa na TICTS ambayo imeingia mkataba wa miaka 25 na serikali wa kupakua na kupakia mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana wakati tunakwenda mtamboni na ambazo hazijathibitishwa, zinasema serikali ya Tanzania iliwahi kutuma ujumbe Costa Rica na Indonesia kutafuta ukweli juu ya Dowans, lakini haikuambulia chochote.
Wasemaji wa wizara ya Fedha, Sheria na Nishati hawakuweza kupatikana kusemea hilo.
Hakuna haja ya kupoteza muda kama tayari mhujumu uchumi anafaamika basi tunamlea wa nini? Jamani tusiendelee kua wajinga enough is enough get rid of him thats it.
This is a legacy of having a corrupt and feeble President.
In year 2005 Kikwete ascended to power through corrupt means of EPA that was executed by the same Rostam Aziz who was the then ruling CCM's treasurer. That scandal that involved stealing billions of monies from the Central Bank to fund CCM election campaigns that put Kikwete to power was later unveiled but the government under the very Kikwete did everything possible to cover the scandal and sabotage investigations and legal processes. In the same scandal RA swindled the central Bank over 40 Billion Tshs through his fake company - Kagoda.
President Kikwete and his corruption infested party CCM has since then been protecting those involved in this scandal and his government was instrumental in assisting the escape of the then Bank of Tanzania Governor Daudi Balali was 'sent for treatment abroad' and did not return, only to be told 'he died there' Kikwete has been paying rhetoric to the fight against corruption and is surrounded by a number of corrupt advisers who include his family.
The problem with the current Constitution is that it allows President to appoint all key players in government including the Judges, Military and Police Leaders, The so called Anti corruption Bureau etc. This effectively makes these organs work faithfully for him and not for the nation.
This explains why all these organs remain numb to all crimes this man has been doing to his country.
To sum up the story Kikwete is a national disaster whose effects can be felt a decade or more after he relinquishes from power.
God Save Our Country.
Heri yao masikini walio huru kuliko matajiri waishio katika utumwa
They might have stolen in the past and escaped judgment. But in this matter of DOWANS & RICHMOND, I swear by the Almighty God, they will never prevail. God is determined to and will judge him/them who are involved.
Mr. Dowans, you are fighting against GOD. GOD will defeat you through the PEOPLE.
EE MUNGU KAMA UPO UNATUSIKIA SISI UTUJIBU HAWA CCM HAWEZI KUENDELEA KUNYANYASA WANYONGE NA MASIKINI NINAOMBA UTUJIBU KWA SABABU WEWE NI MUNGU MASKINI NA WANYONGE
achani kutukana kwani wote mnaonekana wajinga,hapo kinachotakiwa ni kujenga hoja ya jinsi ya kujikwamua kwenye tatizo na sio matusi kwa sababu hayasaidii kitu.
huyu mtu dawa yake ni mchuma tu
I swear nimejiunga na jeshi kwaajili ya kuja kulipiza kisasi kwa ccm, kaeni makao wa kula ni hata kama hawatakuwa viongozi hapo baadae lakini lazima nitimize nililolipanga tena mapema kabla hawajaigawa nchi kwa udini
Kwa kweli hali inatisha Tanzania Kama inafikia Raisi hawezi kufanya chochote mbele ya mtu kama huyu itabidi hata Raisi awajibike haiwezekani Rostam akafanya vitu bila Raisi kujuwa Mungu isaidie Tanzania na watu wake.
Wote mna matatizo ya akili badala ya kuzungumzia kilicho andikwa mnaanza kujibu matusi ama kweli nyani haoni kundule 2mieni hoja jamani sio matusi hayana tija hayo poleni sana ndugu zangu na mungu awatangulie.
Target yao ni 2015
The bad animal of the issue in this scandal is JK. Yeye analipa zile fedha walizotumia na CCM wakati wa uchaguzi wa 2005.
Ndo maana mkakati wao mkubwa kwasasa ni kuhakikisha ya kuwa EL, anakuwa Rais wa 5 wa nchi hii ili awalinde wao na ufisadi walioufanya.
JK, wewe ndo Injinia wa Scandal hii na iko siku utaanguka tuuu.
Mwizi !!!!!!!!!!!!! Auaweeeeeeeeeeeeeee
wewewewewee! uliona wapi wizi akauawa? hayo ndo matatizo yenu, hamna cha maana mnachoandika humu gazetini ila ni kuuana tu, halafu mkijibiwa mnaita watu wehu, sasa hiyo ni akili timamu kweli kumtangazia mwenzako kifo? uuwawe wewe kwanza halafu ndo wengine wafuate.
MWIZI WA MALI ZETU HUYU.
ANAPASWA TU KUNYONGWA HADI AFE !
ananyongwa aliyebainika kuwa ameu, sio mwizi, nyie vipi? yaani mnavyoonekana mmekaa kisharishari tu, sasa unashabikia mwizi auwawe halafu iweje? kama ni mwizi si mumpeleke polisi kisha mahakamani? kuweni na akili acheni ujinga ujinga wa kichaga.
Jamani imefikia kipindi sasa tumkumbuke muumba wa mbingu na ardhi. Kwani yeye ndio muamuzi wa yote tutakayo.
Hawa jamaa wanachofanya leo kesho watakijutia pale damu itakapomwagiga kama tuonavyoona nchi nyingine duniani.
Inakuwaje wewe kama Rais wa nchi uko kimya kwa muda wote, it means kwamba kuna kitu anachokijua kuhusu haya mambo yote ndio mana hata uwamuzi wowote kutoka juu ya hawa wajiitao DOWANS unakuwa mgumu.
Kwa kifupi Rais wa nchi ndio kioo chetu kinachotakiwa kukemea juu ya ukiritimba ufanywao na hawa DOWANS, cha ajabu amekaa kimya. What does it means? tujue anahusika,ahusiki au kwa kuwa yeye anakula na kulala pazuri na familia yake, wanaenda kokote watakapo iwe africa au ulaya? Kikwete angalia uendako, usiache mbachao kwa msala upitao, watanzania engi wanaumia kwa maslahi yenu ya watu wachache mjiitao DOWANS.
HIVI HAKI NA KUJIAMINI KWA ROSTAM KUENDELEA KUFANYA MADUDU HAYA KUNATOKA WAPI KAMA HAKUNA WATU WAKUBWA WANAOHUSIANA NAYE KATIKA KUTIMIZA UWIZI HUU WA MALI NA URITHI WA WATANZANIA? NI UCHAWI GANI AMBAO ROSTAM ANAUTUMIA KUWAFUMBA MACHO RAISI, TAKUKURU, POLISI, CCM NA UONGOZI WOTE WA SERIKALI HII YA AWAMU YA " MAISHA BORA ?" HUYU MTU MMOJA ANAZUNGUMZWA KILA KUKICHA, LAKINI WANAOHUSIKA WAMELALA, HIVI NI KWELI WAMELALA? SIKUTEGEMEA KAMA KUNAWEZA KUWEPO HALI YA SERIKALI KUWEKWA MFUKONI NA MTU, LAKINI HILI LINAWEZEKANA NDILO HASA LILILOPO HAPA. ROSTAM NI BOMU LINALOFUKUTA, NA OLE SIKU LIKIPASUKA, NINA HAKIKA KUWA NDIYO UTAKUWA MWISHO WA CCM. NYIE ENDELEENI TU KUMLEA....
KIKWETE NDO DOWANS WENGINE WOTE WAPAMBE 2. YE NDO AMIRI JESHI MKUU ANGEKUA HAHUSIKI ANGEAMRISHB INTELLIJENSIA ZA KINA IGP ZINGETRACE MPK WANGEMPATA DOWANS TATIZO YEYE JK NDO BOSI WA KAMATI YA tujilie vyetu watz tupa kule. NINA UCHUNGU SANA. ACHENI KUMWONEA HAYA KIKWETE MCHANENI TU YE NDO BOSI. RAIS GANI MWADILIFU HAJAWAHI KUONGELEA ISHU NZITO KA RICHMOND NA DOWANS?
upo sawa sana kiongozi
NCHI YANGU TANZANIA ULISHAKUFA KITAMBO UMEBAKI KUZIKWA TU.
MIMI NINAAMINI IPO SIKU WATU WATACHINJWA KAMA KUKU.
HAWA WAASIA, WAKIONGOZWA NA ROSTAM,MANJI NA WENGINEO IPO SIKU WATALIA MBELE YA HALAIKI. KAZI YAJA
Watanzania tumejengwa katika huruka ya kustahimiliana, ninin kinachosababisha hari hii chafu ya kutukanana?, ni watu kumchoka mtu ama ni huu tunaouita atandawazi, hapana ni matumizi mabaya ya mamalaka tunazopewa, natakakusema neno moja ambalo ningependa kila mmoja aelewe kuwa anatakiwa kuwajibika upande wake, Mtawala na lmtawaliwa wote hawatakiwi nchini mwetu ni kwanini sasa wanakuwepo?, hii hari yakuwepo wapingania haki kwenyenchi yenye hari inayotajwa kuwa ya usawa usioonekana, tuliouenzi kwa viongozi waliopita ndo huu uliopo sasa?. Jiulize ni kweli watanzania tuna ummoja kweli kama tunavyodanganyana?,Je kwanini tunategeana kwenye maamuzi yenye manufaa kwa taifa, nasema tuntegeana nikiwa na ushahidi, kwanini tunasema kesho wafanyakazi wa .........., tuagoma kwaajili ya manufaa yetu, wote tunitikia pooowa, kesho wanaonekana 2% tu ndo wanaonekana. sasa tunaongelea suala la Katiba wote macho juu ngoja tuambiwe tutoe mawazo yetu watu bize, mwisho utasikia jamaani akina Rostam, Lowasa, na wengine mtawataja kuwa watawauwa, je mnataka waamue kwa faida ya nani kama ninyi hamtaki masilahi yenu kuyatetea.Mwisho nakupa uhakika ambao utauona hapa punde kesho tangaza maandamano Arusha uone wangapi watajitokeza, Je ni kweli watanzania ni wamoja?
Uko sahihi OMBI langu kwa wahariri pitieni hizi comments kabla ya kuzirusha hewani hii ni aibu na kipimo tosha kua pamoja na kipato cha mtu kidogo alichonacho bado anashindwa kutumia mda wake vizuri hii ni aibu sana kwa mtanzania wa sasa kutukana hadharani tena matusi ya nguono na unayemtukana ni kiongozi wako!!!!kumbuka hata kama hujampatia kura yako kuna binadamu kama wewe(Watanzania) waliompa sasa iweje utukane hadharani hivyo je ni kuonyesha kua unahasira au ni jinsi gani ulivyo na uwezo mdoga wa kufikiri yaani nashindwa huyo jamaa kumfananisha na chochote???!!!masikiniiiiiii mtanzania mwenzetu huyo.....kwa nini unakosa subira mambo hujionyesha hadharani tuuu punguza jazba,Rwanda walikaa miaka kibao kwenye matatizo ya nchi yao lakini sasa hivi respect ya kutosha kabisa na nchi ina kasi mpya ya maendeleo.
mhariri anatakiwa ku moderate page hii,tunaona lugha kali na za matusi zinatumika humu,hasa kwa wachangiaji wawili wa kwanza kwa kweli si ustaarabu kutumia Lugha ya matusi kiasi hiki!loh!! tujifunze kutukana lakini sio kwa matusi makali kama haya!!inawezekana kabisa kuandika maoni yako bila kutukana matusi ya nguoni kiasi hiki!!this is too much
ni kweli ndugu yangu, ni matusi makali sana, ila siku zote huwa hivi: ukimtukana mzazi wa mwenzako na yeye atamtukana mzazi wako, mimi naona huyu mtukanaji wa pili ametukana baada ya wa kwanza kutukana, sidhani kama huyu wa pili angetukana kama huyu wa kwanza asingetukana, anatakiwa kubadilisha lugha yake la sivyo ataendelea kutukanwa yeye na hao anaowatetea.
Ukweli unaouma,
Rostam Aziz ndiye rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Kikwete kivuli tu.
Rostam Aziz anauraia wa nchi zaidi ya tatu...na anapasport tatu.Rostam Aziz ni mafia
swali....tumuadhibu vipi????????
you know fellow Tanzanians I been diggin bout the matter for quite sometime. ever since RICHMOND got caught back in 200... have you ever heard any comment or a single word frm KIKWETE? bas iyo ndo DOWANS na RICHMOND. J.K ndie kila kitu ktk sakata hili hana la KUSEMA coz ye ndo BOSS mnafiki mkubwa. Rais gani aweza kaa kimya kwny heauy matter kama hii? Ngeleja,Rostam,Jk wote ni STAKEHOLDERS. sasa watz 2livokuaga nyuma tunawalaum wasaidizi wanaofanya STRUCTURED DECISIONS wkt bos yupo na ye ndo anafanya UN STRUCTURED DECISIONS? Tuamke wananchi tudai haki yetu. Nchi gani hii wananchi wamelala km pono! mi naudhika kweli VIONGOZI WA TANZANIA HAWASIKII BILA KUWALAZIMISHA KWA MAANDAMANO. Tuweni na moyo km MARTIN LUTHER R.I.P
hivi hao dowans si wanaaccount,nandiyo watakayolipiwa au watapewa hela cash,ni nani atakaye zipokea,account ya nani na wasipompa nini kitatokea.
Mwizi ajulikanaye kuwa anaiba na papo akaachiwa aendelee kuiba huwa hajiibii peke yake bali ni dalai tu anayejiibia na kuiba kwa niaba ya wenziwake wakuu!
Mwizi ajulikanaye kuwa anaiba na papo akaachiwa aendelee kuiba huwa hajiibii peke yake bali ni dalai tu anayejiibia na kuiba kwa niaba ya wenziwake wakuu!